Huenda
ukiambiwa utaje wanyamapori hatari sana duniani, kwa haraka haraka utakimbilia
kwa simba ama chui kwa haraka au tembo.
Nyegere
ama Honey badger ni miongoni mwa wanyamapori hatari zaidi duniani. Kwa tarifa
yako tu hata nyoka, chui na simba huufyata kwa Nyegere.
Nyegere
ndio mmoja kati ya wanyamapori wasioogopa kitu chochote duniani, huweza
kuwakabili simba na chui zaidi ya mmoja na kuwashinda. Na yeye hategemei mob
kwani ni mmoja wa wanyamapori wanaotembea kivyake wakati wote isipokuwa wakati
wa kupandana tu.
1:Nyegere
ana gozi ngumu zaidi kuliko wanyamapori wote wa mwituni kiasi ambacho ni ngumu
sana kumuua kwa mshale au hata panga, gozi la mnyama huyu linafanya sindano ya
nyuki kudunda tu, anasaidiwa na kucha zake ndefu na ngumu awapo katika hatari
ya kushambuliwa ambapo ngozi yake huwa ngumu na kukakamaa zaidi (defensive
mechanism)
2:
Nyegere hula vyote iwe nyama iwe majani na hii imemfanya kustahimili shuruba za
mazingira yote iwe nyikani ama mwituni. Chakula chake kikubwa ni asali, yeye
hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote
hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.
Nyegere
hula nyoka wa aina yoyote, ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote
haponi. Ingawa wapo nyoka wengi wenye sumu ambao Nyegere akiwala anaweza
kuzimia kwa msaa kadhaa kutokana na ukali wa sumu ambayo inakuua wewe kwa
dakika tu
3:
Nyegere ni moja kati ya wanyamapori wenye wivu sana hapa duniani kwani ana wivu
na mapenzi makubwa sana kwa jike lake. Hutembea nyuma ya jike huku akiwa
ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likigusa sehemu ya siri ya jike
litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wake ni kuwa jani nalo
laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.
Wivu
wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu na hasa wanaume.
Mwanaume
ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano,
huona wivu kuwa utamtamani jike lake, hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu
za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
4.
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, warina asali ndio
waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere, anaweza kuujambia mzinga akala kidogo
asali na kupeleka kwa mke wake. Mrina asali akifika na kupakua, nyegere
ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na
akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake
(ukizingatia milango ya vijijini si imara) na watu wengi vijini wameuwawa kwa
namna hii
Ogopa
sana kukutana na mnyamapori mwenye wivu ambae ni Nyegere...
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyerina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, lakini akabagua yule mwizi wake tu, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyerina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, lakini akabagua yule mwizi wake tu, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
Hiyo
ndiyo sayansi ya Nyegere
Post a Comment