Na: Sylvester Raphael
Kutokana na usimamizi na uongozi thabiti chini ya Mkuu wa
Mkoa mahili wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salum M. Kijuu kiwango cha Elimu mkoani
hapa kimeanza kupanda kwa kasi na kuifanya Kagera kuanza kurejerea katika miaka
ya 1980 wakati ule mkoa ulipokuwa unasifikakwa jina la “Nshomile”
Katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2016 Mkoa wa Kagera
umeendelea kufanya vizuri na kushika
nafasi ya tano kati ya mikoa 10 bora, Aidha mwaka 2014 Kagera ilishika nafasi
ya 10 kati ya mikoa kumi bora, mwaka
2015 mkoa ulishika nfasi ya 7 kati ya mikoa 10 bora na mwaka huu umepanda juu
nafasi mbili za ufaulu.
Halmashauri iliyoongoza katika mkoa wa Kagera ni Ngara iliyofaulisha
kwa asilimia 87.82% na kitaifa imekuwa ya 12, mwaka jana 2015 ilikuwa ya 18. Ya
pili ni Biharamulo iliyofaulisha kwa asilimia 85.11% na kitaifa imeshika nafasi ya 21, mwaka jana
ilikuwa ya 3. Halmashauri ya tatu kimkoa ni Muleba liyofaulisha kwa asilimia
83.69% na kitafa kushika nafasi ya 24 ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya
43.
Halmashauri ya nne ni Manispaa ya Bukoba iliyofaulisha kwa
asilimia 83.23% na kushika nafasi ya 26 kitaifa aidha, mwaka jana ilishika
nfasi ya 47. Ya tano ni Missenyi liyofaulisha kwa asilimia 78.80% na kushika
nafasi ya 46, mwaka jana ilikuwa ya 19. Kyerwa ya sita imefaulisha kwa asilimia
77.60% na kushika nafasi ya 53 ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya 68
kitaifa.
Karagwe ya saba iliyofaulisha kwa asilimia 76.79% na kushika
nafasi ya 54 kitaifa ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya 72 kitaifa.
Halmashauri ya mwisho ni Bukoba iliyofaurisha kwa asilimia 74.86% na kushika
nafasi ya 69 kitaifa ambapo mwaka jana ilishika nafasi ya 102, aidha, imepanda
nafasi 33 kitaifa japo imekuwa ya mwisho katika mkoa wa Kagera.
Shuleiliyoongoza mkoani Kagera na kuwa katika shule 10 bora zilizofanya vizuri
kitaifa ni St. Achileus Chiwanuka kutoka
Wilaya Muleba .
Akiongelea matokeo hayo Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Aloyce
Kamamba alisema mkoa wa Kagera unaendelea kufanya vizuri na miaka ijayo mkoa
huu utaweza kushika nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa zamani. Aidha, Afisa Elimu
kamamba alisema yeye na wataalam wake watafanya tathmini ya kina kujua kwanini
Halmashauri ya Biharamulo imeshuka katika ufaulu ukilinganisha na mwaka jana .
Bw. Kamamba aliipongeza Halmashauri ya Bukoba kuwa pamoja na
kushika nafasi ya mwisho katika mkoa kama mwaka jana lakini imepandisha asilimia
za ufaulu aidha, imepanda nafasi 33 kitaifa. Bw. Kamamba alisema kuwa juhudi za
walimu zimeonekana lakini akatoa wito kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha
inaongeza juhudi ili iweze kutoka nafasi ya mwisho kimkoa.
Katika hatua nyingine Afisa Elimu Bw. Kamamba alisema mkakati
wa mkoa ni kuhakikisha Kagera inashika nafasi ya kwanza kitaifa ambapo yeye
pamoja na timu yake ya Elimu chini ya uongozi wa mkuu wa Mkoa wa Kagera
wataendelea kufanya usimamizi wa kina ili kuhakikisha kiwango cha elimu
kinaendelea kupanda mkoani Kagera.
Mikoa kumi iliyofanya vizuri kitaifa ni Geita iliyofaulisha
kwa asilimia 86.92% mwaka jana 2015 ulishika nafasi ya 6. Wa pili ni katavi
uliofaulisha kwa asilimia 86.80%, mwaka jana ulikuwa 1, Iringa ulishika nafasi
ya 3 na ulifaulisha kwa asilimia 82.87%, mwaka jana ulikuwa wa 10. Dar es
Salaam umeshika nafasi ya 4 kwa kufaulisha kwa asilimia 82.59%, mwaka jana
ulishika nafasi ya 2. Kagera numeshika nafasi ya 5 kwa kufaulisha kwa asilimia
80.99% na mwaka jana ulishika nafasi ya 7.
Mkoa wa sita ni Mwanza uliofaulisha kwa asilimia 79.13%, mwaka
jana ulikuwa wa 3 kitaifa. Kilimanjaro
umeshika nafasi ya 7 na kufaurisha kwa asilimia 79.10%, mwaka jana ulikuwa wa
4. Arusha umekuwa wa 8 kwa kufaurisha kwa asilimia 77.58%, mwaka jana ulishika
nafsi ya 5. Njombe umekuwa wa 9 kwa ufaulu wa asilimia 77.10% na mwaka jana
ulikwa wa 9. Tabora umekuwa wa 10 kwa ufaulu wa asilimia 71.35% na kushika nafasi ya 10aidha mwaka jana ulikuwa mkoa wa 25, wa pili kutoka
mwisho.
Post a Comment