Mwenyekiti wa Baraza
la Nyumba na
Ardhi wilaya ya
Karagwe Logat Asei amewahakikishia wananchi
kuwa chombo hicho
kinatenda haki katika
kutekeleza majukumu yao
ya kila siku
hivyo kuwataka kuondoa
shaka wanapofungua mashauri yao.
Mwenyekiti huyo
ametoa kauli hiyo leo alipotembelea eneo
la mgogoro wa
ardhi kati ya
Agnes Mukuta na Anderea
Mburumwina katika kata
ya Nyakahanga ambao tayari baraza
la nyumba na
ardhi Bukoba lilishatoa
hukumu yake Novemba 20,2015 .
Asei amesema katika
kupunguza migogoro ya
ardhi baraza la
nyumba na ardhi
litakuwa linachukua muda mfupi
kutoa uamuzi wa
mashauri yanayofunguliwa ili
kuepusha kuongeza ukubwa
wa tatizo.
Kwa upande
wake Agnes Mukuta
akionesha vielelezo vyake kudhibitisha umiliki
wa eneo hilo ametoa nyaraka
zinazoonesha hukumu
zilizotolewa kuanzia ngazi ya
kijiji hadi Baraza la Nyumba
na Ardhi Bukoba
alishinda shauri hilo
licha ya utekelezaji
wake kuchelewa.
Aidha, baada ya
kifo cha Andrea Mburumwina
aliyekuwa mlalamikiwa ,kijana
wake Kombe Anderea alidai kuwa ardhi hiyo inayolalamikiwa aliinunua
kutoka kwa mkazi mmoja aliyemtaja kwa
jina moja la Karashani.
Post a Comment