Zaidi ya
wajasriamali mia moja kutoka
maeneo mbalimbali ya
wilaya ya Karagwe,Kyerwa na
maeneo mengine ya
mkoa wa Kagera
wamejitokeza mafunzo ya siku
mbili ya kilimo cha
Uyonga yanayofanyika mjini
Kayanga ambayo yanaratibiwa
na Uongozi wa
Redio ya Jamii Fadeco.
Katika mafunzo
hayo Wajasriamali wameshauriwa kutumia madhalia ya Mimea
mbalimbali ili kusaidia katika uzalishaji wa zao la Uyoga hali itakayowasaidia kuongeza kipato na
kuinua uchumi wao, Wilaya, Mkoa na
Taifa kwa ujumla.
Mkurufunzi wa mafunzo hayo ni ABRAHAM KARONGA amesema kuwa wananchi wanaweza kutumia mazalia ya mimea
kwa shuguli ya uzalishaji uyoga bila kutumia gharama kubwa hali itakayowasaidia kuzalisha zao hilo kwa
wingi huku akiwataka watubutu na kufanya
kilimo hicho cha Uyonga na
shughuli nyingine.
Karonga amefafafanua faida
za Uyoga ni kuongeza vitamin D, na kutibu magonjwa
malimbali ikiwemo kansa na shinikizo la damu huku akieleza kuwa ni chanzo cha
kuwaingizia kipato bila kutumia mtaji mkubwa.
Kwa upande wao wajasriamali walioudhulia
mafunzo hayo wamesema kuwa wamewafumbua kiakili kwa mafunzo waliopata kwani wengi wao
walikuwa hawajui umuhimu wa zao hilo na jinsi ya kuulima.
JASPER ZINGILAMA amesema kuwa amenufaika na mafunzo na mafunzo hayo kwani
katika maisha yake alikuwa akifikili uyoga haulimwi bali un atokana na wanyama
mbalimbali kama nyoka.
Aidha FROLENCE KAHWA
amesema kuwa wajasriamali hawanabudi kutumia fursa hii ili kufanya miradi mbalimbali na kuhudhulia
mafunzo yanayotokea ili kupata ujuzi na
kufanya miradi yenye ubora.
Hata hivyo wadau wote kwa
pamoja wameushukuru uongozi wa wa Redio
ya Jamii Fadeco kwa kuwaletea
wakurufunzi mbalimbali kwa lengo la kusaidia huku wakisema kuwa wataenda
kuthubutu na kufanya kutokana mafunzo wanayoendelea kupata.
Post a Comment