Halimashauri
ya Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera imeagiza tani 20 za Mahindi zilizotakiwa kwa ajili ya msaada
kutoka ghala la kuu la taifa kwa watu
wanaokabiliwa na janga la njaa na tani139
zitakazokuwa zinauzwa kwa bei nafuu.
Hayo
yamebainishwa na Afsa kilimo Wilaya hiyo
KAVITA SALUMONI wakati alipokuwa akitoa taarifa kaita mkutano
wa baraza la madiwani wakati wakijadili
Agenda namba sita iliyowekwa kwa dharura kwa ajili ya upatikanaji wa chakula .
SALUMONI
amefafanua kuwa halimashauri hiyo imeagiza tani 20 kwa ajili ya msaada kwa
wananchi na tani 139 zitakuwa zinauzwa kwa kilo shilingi 50 ili kuwanusuru
wakazi wa wilaya hiyo na janga la njaa linalowakabili.
Aidha
ameongeza kusema kuwa katika kukabiliana na hali ya ukame inayoendelea wilayani
humo madiwani katika baraza hilo wameagizwa kuruhusu wananchi kulima kwenye
tingatinga mazao yanayokomaa kwa mda mfupi ili kuondokana na janga hilo huku
wakionywa wananchi hao kuto lima kwenye mabonde ya hifadhi ya misitu na vyanzo
vya maji.
Nao madiwani walokuwa wamehudhulia katka
balaza hilo wameunga mkono wazo hilo na kumuomba mkurugenzi wa halimashauri
hiyo kuhakikisha chakula hicho kinasambaa kwa walengwamara kitakapowasili.
Hatahivyo
Wakati hoja hizo zikijadiliwa madiwani hao wamesema kuwa 27 mwezi huu mvua
imenyesha kwa baadhi ya maeneo hali iliyopelekea kuwapa matumaini wakulima kwani walikuwa tayari wamepoteza matumaini ya
mvua kutokana na jua lilivyokuwa likiendelea kuwaka kwa kasi wilayani humo.
Post a Comment