Na: Sylvester Raphael
Maafisa Ustawi wa Jamii
Tanzania waliosoma Shahada ya Sosholojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia
mwaka 2001 na kuhitimu Mwaka 2004 wameonyesha mfano wa kuigwa na wahitimu wa kada
mbalimbali kwa umoja wao ambao umetoa mifuko tisini ya saruji kusaidia
waathirka wa tetemeko mkoani Kagera.
Akitoa msaada huo Kwa Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum M. Kijuu kwa niaba ya wenzake Afisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kagera Bi Rebbeca Gwambassa alisema kuwa walihitimu Shahada ya Sosholojia chuo Kikuu
cha Dar es Salaam mwaka 2004 na wana kundi la mtandao wa kijamii la WHATSAPP
ambalo limeguswa na janga lililotokea mkoani Kagera na kuamua kuchangia.
Bi Rebbecca alisema kundi
lao lina Maafisa Ustawi wa Jamii 100 na walichangishana na kufikisha kiasi cha
shilingi 1,520,000/= ambazo waliamua kununua Saruji mifuko 90 na kuikabidha kwa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ili iwasaidie waathirika wa tetemeko kwa kurudisha
miundombinu iliyoharibiwa.
Aidha, Bi Rebbecca alisema
kuwa wao kama wataalamu wa masuala ya kijamii wameamua kutoa msaada huo kwa kuonyesha mfano kwa wanataaluma wengine kuwa
mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika kwa kuleta mabadiliko kwenye jamii na
siyo kuitumia mitandao hiyo kwa mambao ambayo hayana faida katika jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Kijuu akipokea msaada huo aliwashukuru wanataaluma hao na kwakuonyesha mfano
hasa kupitia katika umoja wao wa kundi la Whatsapp kwa kuchangishana na kutoa
msaada wa mifuko 90 ya saruji kwa ajili ya kuwasaidia Wanakagera .
“Kama kila kundi la Whatsapp
hapa nchini likiamua kuchangia kidogo kidogo hata mifuko kumi tu ya saruji
wananchi wa Kagera watakuwa wamepata msaada wa kutosha. Ninatoa wito kwa
wanataaluma wengine kupia makundi yao mbalimbali ya mitandao ya kijamii kujitoa
kama kundi la Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania walivyoonyesha mfano katika
kuchangia maafa Kagera .” Alisistiza Mhe. Kijuu.
Hadi sasa mkoa wa Kagera
umepokea misaada ya mahitaji mbalimbali yenye thamani ya shilingi 1,700,000,0000/= ambapo tayaria miundombinu mbalimbali kama
shule, zahanati, vituo vya afya na barabara
imeanza kujengwa ili wananchi warejeshewe huduma za kijamii.
Katika hatua nyingine Tume
ya ushindani Tanzania imetoa msaada wa msaada wa mabati 5,743 sawa na bandari
360 yenye thamani ya shilingi 86,145, 000/=. Pia na shirika la KADERES la
wilayani Karagwe kupitia shirika la Direct Relief la nchini Marekani wametoa
madawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya 40,000,000/=
Post a Comment