Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: MKURUGENZI MTENDAJI WA KARAGWE KATEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA MULEBA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
Aliyekuwa   mkurugenzi   Mtendaji   wa   halmashauri   ya   wilaya   ya   Karagwe   Richard   Henry   Ruyango   ameteuliwa   kuwa   Mkuu...

Aliyekuwa  mkurugenzi  Mtendaji  wa  halmashauri  ya  wilaya  ya  Karagwe  Richard  Henry  Ruyango  ameteuliwa  kuwa  Mkuu  wa  wilaya  ya  Muleba  huku  aliyekuwa  mkuu  wa  wilaya  Deodatus Lucas  Kinawiro  akihamishwa  kituo  cha  Kazi  na  kuwa  mkuu  wa  wilaya  ya  Bukoba  mkoani  Kagera.



Katibu Mkuu  Kiongozi  Balozi  John Kijazi amesema  katika  uteuzi  huo  Rais  Magufuli  amewateua  wakurugenzi 22 ambao  wameonesha  kufanya kazi  kwa  bidii  huku  wakuu  wa  wilaya 39  wakibakizwa  kwenye  uteuzi  wao  kwa  kubadilishwa  vituo  vyao  vya  kazi  huku  sura  mpya  za  vijana  zikitawala  kwenye  uteuzi  wa leo  na  mtangazaji  wa  kituo  cha  television  cha  ITV  GODWIN   GONDWE  akiteuliwa  kuwa  mkuu  wa  wilaya  ya Handeni  Mkoan  Tanga.


Balozi  John  Kijazi  amesema  kuwa  katika  uteuzi  huo   Rais  Magufuli  amezingatia   mambo  kadhaa  ikiwa  ni  pamoja  na  umri   ambapo  wale  ambao  umri  wao  ni  zaidi  ya  miaka  60  ameamua  wastaafu,amewashukuru  kwa  sana  kwa  utumishi  wao  mzuri na  amesema  pale  itahitajika  serikali  itaendelea  kuwatumia  katika  majukumu  mengine.

Aidha  nafasi   78 za  uteuzi wa  wakuu  wa  wilaya  zimejazwa  na  Watanzania  wengine  ambao  wameteuliwa  kwa  mara  ya  kwanza  wengi  wao  wakiwa  ni  vijana  wenye  elimu  ya  kutosha  na  uzoefu   katika  maeneo  mbalimbali.

Katika  mkoa  wa  Kagera  wakuu  wa  wilaya  wapya  walioteuliwa  ni  Wilaya  ya  Karagwe  ni Geofrey Muheluka Ayoub ,Kyerwa  ni Kanali Shabani  Ilangu Lissu,Biharamulo ni Saada Abraham Mallunde,Missenyi   ni  Luten Kanali Denis F.Mwila  na  wilaya  ya  Ngara  ni Luten Kanali Michael  M. Mtenjele.


Aliyekuwa  Mkuu  wa  wilaya  ya  Missenyi Festo  Sheimu  Kiswaga   amehamishiwa  Bariadi  Mkoani Simiyu  huku  Dary  Ibrahimu  Rwegasira wa Biharamulo , Luteni  Mstaafu  Ole  Lenga wa Kyerwa ,Honoratha  Kitanda wa Ngara ,Jackson Masome wa Bukoba  na Fransis Isaack   wa  Muleba  wameachwa  kwenye  uteuzi  huu.


Hata  hivyo   Ruth  Blasio msafiri ,Sumpter  Nshunju Mshama wameendelea  na  uteuzi  wao  kwa  kuhamishwa  vituo  vyao  vya  kazi  ambapo Ruth  Blasio  Msafiri ametoka  wilaya  ya  Kibondo  mkoani Kigoma  wilaya  ya Njombe Mkoani  Njombe  na Sumpter  Nshunju Mshama akitoka  wilaya  ya  Wangong’ombe  mkoani  Njombe  na  kuhamishiwa wilaya  ya  Kibaha  Mkoa  wa  Pwani  ikumbukwe  hawa  waliteuliwa  Oktoba  mwaka  jana  kwenye  kipindi  cha  Kampeini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top