Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo
Juni 26 2016 amefanya mabadiliko
madogo katika safu ya
wakuu wa mikoa na amewateua
wakuu wa wilaya
139 huku uteuzi wa mkuu
wa mkoa wa Mara
Magessa Mulongo ukitenguliwa.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika
mabadiliko hayo Rais
Magufuli amemteua aliyekuwa
mkuu wa wilaya
ya Sengerema Zainabu R. Telack kuwa mkuu
wa Mkoa wa
Shinyanga kujaza nafasi
iliyoachwa wazi na
Anna Kilango Malecela
ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt Binilith Satano Mahenge kuwa
mkuu wa mkoa wa
Ruvuma kujaza nafasi
iliyoachwa wazi na aliyekuwa
mkuu wa mkoa
Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa
ofisi ya waziri
mkuu jijini Dar
es salaam atapangiwa
Kazi nyingine.
Dkt Charles F.Mlingwa
ameteuliwa kuwa mkuu
wa mkoa wa
Mara kujaza nafasi
ya aliyekuwa mkuu
wa mkoa huo Stanslaus
Magessa Mulongo ambaye
uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa
siku ya
jumatano ya juni 29 2016 saa tatu
kamili asubuhi Ikulu
jijini Dar es salaam
na mara baada ya
kuapishwa watakula kiapo
cha maadili ya
uongozi.
Post a Comment