Utamaduni
wa kusifia, bila kukosoa siupendi
Mhariri,
TANGU Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani chini ya Rais John Magufuli
kwa asilimia nyingi imekuwa ni kupongeza hotuba zake utendaji kazi wake hasa
utumbuaji majipu.
Ni kweli usiopingika kuwa Taifa lilikuwa limefikia pabaya kutokana na utendaji
mbovu wa serikali zilizopita kuendekeza uswahiba na kuruhu mianya mingi ya
rushwa,jambo ambalo limetufanya watanzania kugawanyika katika makundi ya
walionacho na wasio nacho.
Lakini pamoja
na uhitaji mkubwa wa Rais wa aina ya Magufuli bado tulihitaji mtu atakaye tumia
busara,umakini diplomasia ya kutosha katika kutekeleza majukumu yake.
Hadi
sasa yapo mapungufu yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano,lakini watu
wanaogopa kuyakosoa wanachokiona nikupongeza tu hii siyo suluhisho la migogoro
bali yatarudi yaleyale yaliyopita, kama unampenda Magufuli basi mkosoe.
Ninaloliona la kwanza tumwambie Rais Magufuli kuwa unatakiwa umakini katika
kupunguza mishahara ya watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za serrikali
inayofikia milioni 45 hadi kufikia milioni 15 baada ya kupunguzwa, bila kufanya
utafiti kuna athari nyingi za kiuchumi zinazoweza kuikumba nchi endapo Rais atatekekeleza
ahadi yake bila kufanya utafiti utakao mpa majibu sahihi.
·
Kitendo kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano kupitia waziri mwenye
dhamana ya habari Nape Nnauye kutoa agiza kwa kituo cha luninga cha Taifa TBC
kutorusha matangazo ya vikao vya bunge moja kwa moja tumweleze Magufuli kuwa ni
ukandamizaji wa vyombo vya habari.
·
Watanzania tusiwe wanafiki tumweleze wazi kuwa tunahitaji utumbuaji majipu
unaofuata kanuni na sheria,hatushabikii lakini kuna lafu nyingi zizochezwa na
wafuasi wake wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa bila kufuata kanuni za utumishi
wa umma.
·
Kukurupuka kwa serikali na kufungia baadhi ya magazeti tumweleze magufuli kuwa
demokrasia haiendi hivyo bali ni kutokana na sheria za magazeti
zilizopitwa na wakati.
Rais wangu John Pombe Magufuli yanawezekana kama utatuletea katiba mpya
iliyokuwa na pendekezo la Jaji Joseph Warioba lakini kwa mtindo huu
hutafanikiwa utaturudisha tuliko toka na yaliyotokea Zanzibar tumeyaona kwa macho.
Na:Mbeki Mbeki
Box 31
KARAGWE.
Post a Comment