Makala
Maendeleo ya wilaya ya karagwe
yako vitabuni siyo mikononi mwa wananchi
Na Mbeki Mbeki
Tunahitaji jamii inayo wajibibika kwa maendeleo yake, maisha bora uchumi
endelevu, huduma bora za jamii na amani kama viongozi wataacha maneno matupu
waka jielekeza kwenye vitendo.
Ukisoma Taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama
cha mapinduzi (CCM) utaipenda hasa ile niliyo pata bahati ya kuisoma ya wilaya
ya karagwe.mkoa Kagera.
Maendeleo na mafanikio yanayo zungumzwa yako vitabuni wala hayafanani na hali
halisi ya wilaya ya karagwe yenye ardhi nzuri,mifugo mazao ya kila aina na
vivutio mbali mbali vya kitalii.
Inasitikisha kwa wilaya kama ya karagwe ambayo kihistoria ilianza mwaka 1961
nahadi sasa imeongozwa na wakuu wa wilaya 19 hadi kufikia mwaka huu haina kituo
cha magari (stendi) uwanja wa michezo, shule ya kidato cha tano na sita wala
chuo kikuu hata kimoja.
Wilaya ya karagwe ina eneo la kilometa za mraba 4,500 kati ya hizo kilometa za
mraba 4,342 nieneo la inchi kavu na kilometa za mraba 158 ni eneo la maji
na eneo linalo faa kwa kilimo ni Hekta 153,540.
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012
wilaya ya karagwe ilikuwa na jumla ya watu 332,020 kati ya hao
163,864(wanaume)na 168,156 (wanawake)ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.9.
Aidha uzalishaji wa zao la kahawa umefikia tani 8,100 kwa mwaka 2015 na miche
526, 000 ya kahawa imezalishwa kwenye vitalu vya wakulima na makampuni
binafisi na kugawiwa kwa kulima sawa na asilimia 52.6.
Kuongezeka kwa eneo linalo limwa mazo ya chakula na biashara kwa wilaya karagwe
kutoka hekta 61,000 kwa mwaka 2010 hadi hekta 82,808.5 mwaka 2015
kunatokana wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbadala kama Alizeti,maharage
tofauti na kahawa na migomba.
Lakini maendeleo yanayo zungumuzwa katika ilani yana paswa kuonekana kwa macho
siyo vitabuni ,tutakuwa tunajidanganya kama wanafika viongozi wa juu
tunawasomea taarifa hewa kama zinavyo onyesha kwenye vitabu vyao.
Wilaya imeanzisha
mradi mkubwa wa umwagiliaji katika kijji cha Bujuruga kata ya Bugene ambao
umegharimu kiasi cha shilingi milioni 600,000,000 wenye hekta 250 tangu mwaka
2009 hakuna jipya linalo onekana pale.
Mkuu wa wilaya ya karagwe Deodatus kinawilo anasema
mradi wa umwagiliaji haujakamilika kwa kuwa fedha zilizo kuwa zimetengwa
kwa ajili za mradi huo madiwani walizigawana na kulipana posho.
Anasema
ofisi yake ilimwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kuzirudisha
kutoka kwanye vyanzo vya ndani vya Halmashauri ili mradi uendelee.
Kinawilo
anasema hadi sasa kiasi cha shilingi milioni 274.7 zimeisha rudishwa na
kuwa baada ya utafiti wa pili walibaini mradi huo haukuwa na
thamani ya shilingi milioni 600,000,000 bali gharama ya mradi ni shilingi
milioni 433.
Hata hivyo Kinawilo anaeleza kuwa fedha zinazo kuwa zimelengwa kwenye
miradi mbali mbali zimekuwa ziki badilishwa matumizi kulingana na mahitaji
makubwa ya wakati huo.
Anasema milioni 120 zilizo kuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa
michezo zilielekezwa kwenye ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.
Uwanja huo ulianza ujenzi kati ya mwaka 2009/2010 na sasa hivi umegeuka kuwa
uwanja wa kujifunzia magari una uhusiano gani na ujenzi wa maabara mwaka
2015? Wananchi wanahoji
Wakazi wa wilaya ya karagwe hawatashangaa tabia ya viongozi wao kubadili miradi
inayo kuwa imebuniwa na wananchi na baadae viongozi kuiteka
nakuibandika miradi wanayo itaka wao hili limekuwa ni jambo la kawaida katika
wilaya ya karagwe.
Wakitolea mfano ujenzi wa chuo cha ualimu cha karagwe ambacho bila
kushirikisha wananchi waliotoa ardhi kimebadilishwa na kuwa shule
ya mchepuo wa sayansi kidato cha tano wasichana bila kushirikisha
wananchi walio kuwa wameibua mradi huo.
Mdau wa maendeleo Clement Nsherenguzi amesema tabia ya kubadirisha
matumizi ya mradi iliyoibuliwa na wananchi inawakatisha tamaa wananchi
wapenda maendeleo
“viongozi wanaandika kuridhisha waliojuu yao nakutugeuza sisi kama
watu wasioelewa, miradi gani isiyokamilika zaidi ya miaka kumi?”.Anahoji
Nsherenguzi
Anasema mradi wa umwagiliaji wa Bujuruga haukuibuliwa na wananchi
ndio maana wananchi walihitaji fidia baada ya kufyekwa mashamba yao
kuharibiwa vyanzo vya maji walivyo kuwa wanavitegea.
Nsherenguzi anasema haijawahi kutokea mkazi wa karagwe kufikiria kulima zao la
mpunga wakati chakula chao kikuu ni ndizi, kuwa huu mradi ni ulikusudia
kuwanufaisha madiwani kama walivyo gawana fedha za mradi kabla ya kuanza.
Anasema kuwa siyo kweli kwamba wananchi wa karagwe hawataki maendeleo wala
kuchangia shughuli za maendeleo bali tabia za viongozi kutokuwa waaminifu
katika utendaji kazi zao.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri aliandika katika kitabu chake Agost 2015 cha
taarifa ya mafanikio ya utekerezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)
kuanzia oktoba 2010 hadi julai 2015 mambo ambayo wananchi wanazidi kuhoji na
kutoyaona kwa macho.
Anasema uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka 605,441 mwaka 2010 hadi kilo
628,153 za nyama kwa mwaka 2015 lakushangaza nikwamba mwaka 2010 kilo ya nyama
ilikuwa shilingi 2500 na mwaka 2015 kilo ya nyama ni shilingi 5000.
Anasema ukusanyaji wa mapato yatokanayo na minada ya mifugo yameongezeka kutoka
shilingi 34,468,900 mwaka 2010 hadi shilingi 76,526,900 mwaka 2015.
Lakini katika kikao kazi cha mkuu wa wilaya kinawilo mei mwaka huu
alisema ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri uko asilimia 68
na haujafikia kiwango nakuwa sisitiza kuongeza jitihada kukusanya mapato.
Vile vile Mabwawa ya kufugia samaki Richard Ruyango ambaye ni mkurugenzi
mtendaji Alisema mabwawa ya kufugia samaki yameongezeka kutoka 3 kwa mwaka 2010
hadi 67 kwa mwaka 2015 na wafugaji 196.
Kuna maswali ya kujiuliza samaki hawa wanapo ongezeka wanapelekwa wapi?
Wanauzwa wapi? au kama wanasafirishwa ni nchi zipi wanaenda kwani
kuna uhaba mkubwa wa samaki karagwe bei ya samaki ni kuanzia shilingi 5,000
hadi shilingi 10,000 samaki mmoja.
Kila kunapo kucha maisha ya wakazi wa karagwe yanazidi kuwa magumu huku
taarifa ya Ruyango ikionyesha pato la mwananchi kwa mwaka (per
capital income) limeongezeka kutoka shilingi 200,000 na kwa sasa anasema
linakadiriwa kufikia 520,000 hatujui hizi takwimu anazitafiti wapi?
Katika
wilaya yake anasahau kuwa hakuna uongozi shirikishi katika kusimamia
kilimo, upatikanaji na utumiaji pembejeo, utumiaji wazana zana za kilimo
na ushirikishaji wa sekta binafsi kuimarisha mashamba darasa na huduma bora za
ugani.
Post a Comment