Karagwe forum Karagwe forum Author
Title: WAZEE NI HAZINA YA TAIFA WANASTAHILI KULINDWA
Author: Karagwe forum
Rating 5 of 5 Des:
MAKALA       WAZEE NI HAZINA YA TAIFA WANASTAHILI KULINDWA                         Na Mbeki  Mbeki                              ...

MAKALA   
 
 WAZEE NI HAZINA YA TAIFA WANASTAHILI KULINDWA
                        Na Mbeki  Mbeki
                                   Karagwe

               Mwaka 2008 shirika la (ILO) International Labour Organization lilifanya utafiti dhidi ya kupatikana kwa mafao ya uzeeni kwa watanzania na kubaini asilimia 96 ya wazee hawapati kipato chenye uhakika.

          Licha ya masharti kinzani katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania asilimia 96 ya wazee wa Tanzania hawapati kipato chenye uhakika kwa mujibu wa ILO, katika kukabiliana na afya duni na majukumu ya hapa na pale wazee hawakuishi katika umaskini uliokithiri.

     Aidha umaskini wa uzeeni una athari kubwa kwa jamii na kurithishwa kizazi hadi kizazi.

     Katika kukabiliana na hili na hili serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imepiga hatua muhimu katika kuandaa mfumo kabambe wa hifadhi ya jamii.

     Ni kwamba hii ni pamoja na mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) wa sera ya taifa ya usalama wa jamii 2003.

    Kwa upande wake MKUKUTA fungu la 2 lengo la 4 nguzo 43 umebainisha uhitaji wa kutafuta nia ya kutoa hifadhi kwa jamii ya pensheni ya kila mwenzi ili kukidhi mahitaji ya msingi.

     Masharti haya ya sera pia huonyesha dhamira ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kuendana na mfumo wa sera za jamii na umoja wa Afrika kwa ajili ya afrika ambao unalenga kupanua hifadhi ya jamii kwa kutoa kiwango cha chini kwa ajili ya huduma ya lazima ya afya na mafao kwa wazee, watoto, watu wenye ulemavu, wafanyakazi wasio na ajira rasmi na wasio na ajira kabisa.

   Mwaka 2008 wizara za kazi ajira na maendeleo ya ujana (MOLEYD) na shirika la kazi duniani (ILO) walifanya mapitio ya matumizi na utendaji ya hifadhi ya jamii, tathimini hii ilipendekeza kuwa uwezekano wa kuweka pensheni ya uzeeni kwa wote unaopashwa kuchunguzwa kwa kinazaidi.

   Mamlaka ya serikali inapaswa kuweka vigezo sahihi kwa ajili ya utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi,kujielimisha na ustawi wa jamii wakati wa uzee, ugonjwa au ulemavu wa katika namna yoyote ya kutojiweza.

    Aidha pensheni za jamii ni fedha ambayo hulipwa na serikali kwa wananchi wazee tofauti  na pensheni zitokanazo na makato hizi hazihitaji michango yoyote ya awali  kutoka kwa wapokeaji .

      Kwamba badala yake pensheni katika muktadha wa Tanzania huwataka watanzania wote kulipa aina Fulani ya kodi na kutoa mchango wa maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi.

    Pensheni jamii hutoa kipato cha chini na kuhakikisha wazee hawaishi katika umaskini wakati mfumo wa hifadhi wa jamii ni muhimu viwango vya juu vya umaskini ni ukubwa wa sekta isiyo rasmi unaonyesha kwamba mfumo wa mafao yatokanayo na makato hautoshi kupambana na umaskini wa uzeeni kwa Tanzania.

    Pia pensheni za jamii zimeonyesha mafanikiosana kwingineko Afrika mipango ya kimataifa katika nchi kadhaa za kusini mwa Afrika na miradi ya majaribio inayofanyika zambia , Kenya na Uganda .

    Hata hivyo baadhi ya pensheni za jamii hulenga wazee waliomaskini wakati mwingine hutolewa kwa wote waliotimiza umri mwafaka ambao ni miaka 60.

    Ikumbukwe kwa pensheni jamii pia inaweza kuwa pensheni majaribio ambapo mlipwaji hubainishwa na mapato mengine ya pensheni.

     Imebainika kuwa kutokana na mifumo hii umeonyesha kuwa pensheni jamii si tu kupunguza umaskini uzeeni lakini hutoa mchango mpana katika kufikia malengo ya taifa ya maendeleo ya jamii.

     Novemba 2009 hadi April 2010 wizara ya kazi ajira na maendeleo ya ujana (MOLEYD) kwa kushirikiana na Help Age International walifanya uchunguzi wa kina juu ya uwezekano wa upatikanaji wa kipato cha chini kwa wazeee wote.

     Utafiti huu ulihusishwa mashauriano ya kina na viongozi na wadau muhimu katika ngazi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utafiti katika wilaya tatu ambapo tayari kuna mipango midogo ya hifadhi ya jamii kibaha, muleba na chamwino.

     Ripoti hiyo ilianza kwa kutoa mantiki ya kuwepo pensheni kwa wote kwa kuzingatia uchambuzi wa hali ya wazee na kwa kutambua mapungufu yaliyomo ndani ya hifadhi za sasa za jamii,

     Hivyo ripoti hiyo ilitoa matokeo ya uchambuzi wa kitakwimu ju ya umuhimu wa pensheni kwa wote ikizingatia viwango vya maskini Tanzania na kubainisha michango mbalimbali ambayo pensheni kwa wote ingetolewa ili kupanua malengo ya maenedeleo ya taifa yaliyowekwa na MKUKUTA.

    Katibu wa shirika lisilo la kiserikali yaani saidia wazee karagwe (SAWAKA) Livingstone Byekwaso alisema kuwa kuna karibu watu millioni 2 wenye umri zaidi ya miaka 60 na kila kaya moja kati ya nne ina wazee, anaongeza kuwa wazee ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii na uchumi wa Tanzania na ni sehemu muhimu ya Tanzania katika kipindi cha mabadiliko ya haraka ya jamii, kiuchumi na kiutamaduni.

    Hata hivyo alisema uzee una changamoto nyingi ambazo zinakuwa katika mazingira ya Tanzania , wazee wanaa uwezo mdogo wa kujipatia kipato cha kutosha kwa kufanya kazi wanapatwa zaidi na magonjwa sugu na ulemavu na uwezekano mkubwa wa kutengwa na jamii kunyimwa haki na kubaguliwa.

     Byekwaso alisema katika siku za nyuma usalama uzeeni ilitolewa kupitia familia pana na miundo ya kijamii kuwa kutokana na kukosekana na usalama uzeeni kumesababisha kuenea kwa umaskini na kasi ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kusababisha njia za ajali kushindwa kukabiliana na hali.

    Nekemiah kazimoto (81) alisema kuwa kupungua kwa uhifadhi wa jadi kwa wazee unatokana na ukweli kwamba wazee wanadhidi kukabiliana na majukumu ya utunzaji wa familia.

    Alisema asilimia 40 ya yatima watanzania na watoto waishio katika mazingira magumu ambao jumla yao ni takribani million 2 uwategemea wazee kwa mahitaji yao ya chakula, afya na elimu.

     Aliongeza kuwa asilimia 72 ya watoto waishio katika mazingira magumu Tanzania wanatunzwa na wazee ambapo alisema katika hali hii umaskini wa uzeeni una athari kubwa wa familia za wazee hasa watoto.

    Kazimoto alisema viwango vya umaskini miongoni mwa kaya zenye wazee ni asilimia 22.4 zaidi ya kiwango cha umaskini wa taifa na karibu moja ya tatu ya kaya maskini zaidi zina wazee.

     Naye Genegeva Katto (80) mkazi wa kijiji cha Nyamiaga kata ya Bugomola wilaya ya Kyerwa alitaja baadhi ya faida za kuwa na pensheni ya wote katika kubuni pensheni jamii kuwa pensheni kwa wote kwa jamii itakwepa  kuweka motisha kwa jamii, itasaidia wasio maskini wasianguke katika umaskini.

     Alitaja faida nyingine za pensheni kuwa inaweza kutekelezwa kwa bei nafuu kwa kiwango cha taifa, hitaakikisha wazee wote maskini wanafikiwa na kulenga umaskii kutokosa umaarufu wa kisiasa.

    Sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 ilikuwa nyaraka ya kwanza ya kiserikali iliyowekwa bayana haki na ustawi kwa wazee kuwa sera hii ilielekezwa namna ya kukabiliana na matatizo yanayo wakabili wazee na kuyaunganisha katika mkakati wa kitaifa wa kuondoa umaskini.

    Lakini katika mkutano wa wazee na shirika la Help Age International uliofanyika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza Dar-es-salaam ulibainisha kuwa sera hiyo haijatekelezwa na kuwa wazee wanaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

    Akizungumza katika ukumbi huo mkurugenzi msaidizi wa shirika la Help Age International Smart Daniel alisema mwaka 2012 wazee 630 waliuwawa, mwaka 2014 wae 320 na wengi wao wakiwa wanawake.

      Asilimia 96 ya wazee hawako kwenye mfuko wowote  wa hifadhi ya jamii wakiwemo wakulima, wavuvi na wafugaji.

     Hivyo alisema viongozi waliochaguliwa katika nafasi za uongozi yaani udiwani, ubunge na Rais waweke hatua za kuzitatua hizo changamoto na wachukue hatua kulinda haki za wazee.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 

This Template Is Designed By Jacksay | call 0764 031 242 for this service

Top