MAKALA
MariaSalome: Nilipata pesa ya kusomesha
watoto wangu kutokana na biashara ya ngono.
NA: MBEKI MBEKI
Bi Mariasolome Chahola (76) ni mkazi wa
kijiji cha Kasharazi kata ya Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani
Kagera,anasimulia alivvo wasomesha watoto kupitia biashara ya ngono.
Bi Chahola anasema alizaliwa mwaka 1940 kijiji cha Kakuraijo kata ya Kibondo
wilaya ya Karagwe kabla ya kuhamia Chonyonyo alikoko weka makazi yake kwa
sasa.
Ana simulia maisha ya ujana na baadaya kupitia changamoto
mbalimbali katika maisha yake katika nchi mbalimbali alizo tembea ikiwemo
Uganda.
Anasema alihitimu darasa la nne katika shule ya msingi kibondo mwaka 1952
akaanza maisha ya kuishi na wazazi wake kabla ya kutolokea Uganda mwaka 1958.
“Kijana wangu niliamua kwenda Uganda baada ya kuona maisha ya Tanzania yamekuwa
magumu kiuchumi.”
Anasema akiwa Uganda alifanya kazi katika miji mikubwa ya chotela, mbalala
Entebe na Kampala biashara yake kubwa ilikuwa ni ngono katika mahotelimakubwa.
Anaelezea bi Chahola kuwa wateja wake wakubwa walikuwa ni
wabunge na mawaziri ambapo ujira wake ulikuwa ni shilingi 20 hadi shilingi 25
“Na kiasi hicho alikuwa analipwa msichana mwenye umbile zuri na
hasa mimi walinipenda sana wakubwa kwa kuwa nilikuwa najiheshimu ninapo kuwa
nao kulingana na uzito wa kazi zao Anasema Chahola.
Anasema amekuwa katika kazi hiyo ya kuuza mwili tangu mwaka
1965 hadi 1977 kwani alianza kazi ya kuuza baa mwaka 1958 hadi 1965 baada ya
uhuru wa nchi hiyo.
Anasema kazi ya kuuza baa haikumlipa vizuri kama ilivyokuwa ya
ngono ambayo ndiyo iliyo muwezesha watoto wake sita (6) ambao nao aliwazaa kwa
wanaume tofauti.
“Nina watoto sita wakike wawili na wakiume wane ambao
nimewazaa na wanaume tofauti akiwemo mbunge wa kwanza wa karagwe mheshimiwa
Kaneno.
Aidha anasema watoto wake wote wamebahatika kusima shule na
wengine kwa sasa wakiwa wameajiriwa katika ofisi mbalimbali hapa Tanzania na
mtaji wake mkubwa ukiwa umetokana na biashara hiyo.
Anasema akiwa katika kazi yake hiyo alibahatika kufahamiana na viongozi
wengi katika serikali ya Uganda na baadae wenzake wakampendekeza kuwa
mwenyekiti wa wenzake.
Katika kutekeleza shughuri aliyopewa alipaswa kuhakikisha mwanamke
haingilii mpenzi wa mwenzie hasa hasa kulinda maadili yawenzake.
changamoto
Kwa mjibu wa Bi Chahola anasema kuwa changamoto kubwa aliyoipata
kwanza ni ugumu wa lugha ya kiingereza kwani wateja wake wengi walitumia
kingereza na huku ametoka Tanzania akiwa amehitimu darasa la nne.
“Nilijikuta sehemu nilio paswa kujibu ‘YES’ najibu ‘NO’ japo
niliokolewa sana na lugha ya kinyankole ambayo inahusiana na lugha ya yetu ya
kinyambo “Anaeleza Chahola.
Anasema biashara hiyo aliifanya kwa uaminifu mkubwa kwa kuwa
hakuwahi kupigwa ,kufumaniwa au kuwekewa jeraha lolote na mwanamke mwenzie au
mwanaume japo kwa wenzake lilikuwa jambo la kawaida sana.
magonjwa
Anaeleza kuwa kipindi kile hakukuwa na magonjwa ya kutisha kama
ilivyo sasa watu walikuwa wanaambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo yalikua
yanatibika hasa kwa “CAPSULES”
“Sasa hivi nguvu kazi ya Taifa imepotea kutokana na
ugonjwa wa UKIMWI (AIDS) ngono isiyo salama sasa hivi ni hatari kwa maisha
yako”Anasema Bi Chahola.
Anasema anawashangaa vijana wa sasa wanao fikilia suala la mapenzi
na biashara ya ngono wakati haina maslahi yoyotekwao huku wakijua wameathiri
maisha yao.
Anasema hawaelewi vijana wa kike wanao vaa nguo nusu uchi kwa
ajiri ya kutangaza biashara ya miili yao sambamba na wavulana wanao vaa
milegezo ya suluari .
“Nikwambie katika nchi ya Uganda wasichana kwa wanawake
tulivaa nguo ndefu kwa kufunika miguu maarufu kama boarding lakini msichana
kama ni mzuri aliendelea kuonekana na uzuri, nguo fupi ni udharirishaji
haitangazi uzuri”Anasema Bi Chahola
Anasema wanawake wengi wamechubua ngozi wameiga mitindo mingi ya uvaaji kutoka
nchi za magharibi kwa kuchelewa kwani kwa sasa hakuna malipo kutoka kwa
mwana mme
yatakayo kufanya ujenge nyumba au kusomesha mtoto kama ilivyo kuwa awali.
Hata hivyo serikali kupitia bunge inapaswa
kutunga sheria zinazo weza kuwabana watu wanao vaa nguo fupi ili nao wahukumiwe
sawa na wabakaji kwa kuwa nguo zao zina viashiria vya kubaka na kubakwa.
Anasema teknolojia mpya imeharibu watoto kwani vijana
wengi wanaiga mitindo mbalimbali na miziki isiyoendana na maadili ya kiafrika
jambo ambalo limepelekea vijana kuwa wavuta bangi.
“Sikiliza mwandishi pamoja na uzee wangu
aliyetengeneza hizi simu hakuzitengeneza kwa ajili ya mapenzi nafkiri ni kwa
ajili ya watu wenye biashara kubwa kubwa lakini vijana wetu kila wakati
wanachokonoa ukifuatilia ni mapenzi tu na kwamba sasa hivi ni kifo tu wala
hakuna cha mapenzi “Anasema.
Anasema anayo mengi ya kuzungumza na wazazi,walezi na
watoto wa kike kwani pamoja na biashara aliyo fanya ya ngono alijifunza mambo
mengi sana yanayoweza kuwa saidia wale wenye tama ya kujiingiza kwenye
biashara hiyo.
Post a Comment