Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha imetengua ushindi wa Mbunge wa Longido mkoa wa
Arusha,Onesmo Ole Nangole baada ya kujiridhidha kuwa katika chumba cha
majumuisho ya kura hayakua rafiki kuakisi matakwa ya wapiga kura.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba,Sivangilwa Mwangesi amesema licha ya kutupa
ushahidi wa mashahidi wa mlalamikaji 15 na kukubali wanne na pamoja na kasoro
ya kura zenye makosa kutokufikia alizopata mshindi amejiridhisha kutengua
matokeo hayo na mlalamikiwa kulipa gharama za kesi.
Aliyekua
Mbunge wa Longido,Onesmo Ole Nangole amesema alishinda kwa halali na anakusudia
kukata rufaa huku mshindi katika kesi hiyo Steven Kiruswa amesema Mahakama
imetenda haki.
MAHAKAMA
KUU AAA ARUSHA IMETENGUA UBUNGE NA
KUAMURU UCHAGUZ URUDIWE.
Kesi
iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini
Arusha imetolewa hukumu leo hii
Katika
shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido
Dk KIRUSWA alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya
ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh ONESMO NANGOLE.
Akisoma
hukumu hiyo,Jaji MWAGESI
alisema
kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko
Lamwai na Wakili Haraka.
Katika
shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika
kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole
2.Kuwepo
kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika
kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi
wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea
kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana
na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na
vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,
Jaji
kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;
"Kutokana
na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu
wa sheria,Natamka kwamba;
Mahakama
hii imetengua shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa
haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.
Post a Comment