Na: Sylvester Rapahel
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera
na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Kijiji cha Nyakabango mpakani mwa Geita na Kagera ambapo
katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru utapitia miradi ya maendeleo 65 yenye
thamani ya shilingi bilioni 12,385,330,354.
Katika
miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 33, utakagua miradi 19, utaweka
mawe ya msingi katika miradi 13 aidha, mchanganuo
wa gharama za miradi hiyo 65 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama
ifuatavyo, Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi bilioni 5,817,795,968
sawa na asilimia 47%.
Halmashauri
za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi
671,940,497 sawa na asilimia 6%. Aidha wananchi wamechangia shilingi
bilioni 2,181,496,962 sawa na asilimia 17%. Wahisani
wamechangia shilingi bilioni 3,714,096,927 sawa
na asilimia 30%.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 umebeba
kaulimbiu isemayo “Elimu ni
ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli
mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kuwekeza katika
elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla lipate
wataalam wa kutosha katika kada mbalimbali za kitaaluma na hapo taifa letu
litapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani.
Pamoja na Kauli Mbiu tajwa hapo juu Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa
wetu zitaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa,
Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya
na Mapambano dhidi ya Malaria.
Mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu
alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango na Mwenge wa Uhuru
ukaanza mara moja mbio zake wilayani humo za kukagua miradi ya maendeleo.
Akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio hizo Charle
Francis Kabeho katika eneo la Nyakabango aliwasisitiza wanafunzi kusoma kwa
bidii masomo ya Sayansi kwani Serikali imefanya kazi yake ya kujenga shule na
vyumba vya mahabara na kuweka vifaa vya kutoasha katika maabara hizo
Post a Comment