Na: Sylvester Raphael
Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa
kuendelea kuzindua, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kutembelea miradi
mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya za Karagwe na Ngara.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mwenge wa Uhuru
ulikimbizwa Wilayani humo tarehe 13 Aprili, 2018 ambapo jumla ya miradi 12
ilipitiwa na Mwenge wa Uhuru na kukagua, kuizindua, kuweka mawe ya msingi na
kuona uendelevu wa miradi iliyopitiwa na Mwenge huo mwaka jana 2017
Katika Miradi hiyo 12 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani
Karagwe wananchi walichangia kiasi cha shilingi 1,339,482,000/=, Halmashauri
shilingi 28,085,600/=, Wahisani shilingi 789, 234,132/=, na Serikali Kuu
shilingi 766,578,211/= ambapo thamani ya miradi yote jumla ni shilingi
3,175,124,660/=.
Mwenge wa Uhuru umeendelea na mbio zake leo Aprili 14, 2018
Wilayani Ngara mara baada ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Michael
Mtenjele kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka.
Ukiwa Wilayani Ngara Mwenge wa Uhuru umeweza kuipita miradi ya
maendeleo yenye thanmani ya shilingi bilioni 207,026,400/= katika Sekta za
Kilimo, Elimu, Huduma za Jamii kama Afya na Maji, pamoja na miundombinu ambayo
ni barabara.
Ukiwa Wilayani Biharamulo April 15, 2018 Mwenge wa Uhuru
ulipitia miradi ya maendeleo ipatayo sita na yenye thamani ya shilingi milioni
917,976,109/=
Akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge Wilayani humo Kiongozi wa
Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho aliwasisitiza wananchi
kuwekeza katika Elimu ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Aidha, aliwasisitiza
wananchi kuhamasika katika shughuli za kiuchumi ili kujiletea maendeleo na
kuachana na shughuli zisizokuwa na tija kama kujihusisha na kilimo cha bangi
ambayo ni madawa ya kulevya.
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake mkoani
Kagera utakabidhiwa Mkoani Kigoma tarehe 16 April, 2018 ili kuendelea na mbio
zake mkoani humo.
Post a Comment