Na: Sylvester Raphael
Vyombo ya Ulinzi na Usalama
Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya pamoja ili kijiweka tayari na kushirikiana
kwa pamoja katika kutekeleza jukumu moja kuu la kuwalinda raia na mali zao.
Mazoezi hayo yaliyofanyika
katika Manispaa ya Bukoba Aprili 25, 2018 yameyashirikisha Majeshi ya Polisi,
Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, Jeshi la Akiba na Jeshi la Wananchi Tanzania.
Akiongea na Waandishi wa
Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Olomi mara baada ya
kuhitimisha mazoezi hayo katika Viwanja vya Gymkhana alisema kuwa ni mazoezi ya
kawaida kwa Majeshina kitaalam yanaitwa (Route Match)
“Mkoa wa Kagera tumekuwa na
utaratibu wa kufanya mazoezi haya kila Jumamosi ya kila wiki kwa kushirikiana
na wananchi lakini leo wananchi wapo kwenye shughuli zao za uzalishaji, Majeshi kama unavyoyaona tumeshirikiana
kufanya mazoezi ya pamoja kwani sote jukumu letu ni kulinda raia na malizao,” Alifafanua
Kamanda Olomi
Aliongeza Kamanda Olomi kuwa
Majeshi yakifanya mazoezi ya pamoja wanakuwa na utayari wa pamoja kupambana na
vitendo ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama wa raia na mali zao lakini pia na
Askari katika mazoezi haya wanafahamiana kwa karibu jambo linaloleta
ushirikiano mzuri katika kazi.
Aidha, Kamanda Olomi
alitumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wale wote wanaopanga kundamana au kufanya
vitendo vya uvunjifu wa amani siku ya maadhimisho ya Muungano tarehe 26 Aprili,
2018 kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera limejipanga vizuri kushughulika nao
kikamilifu.
Kamanda Olomi alisisitiza
kuwa mwananchi yeyote asidanganyike kwa kushawishiwa kuandamana na aliwataka
wananchi hao kuendelea na shughuli zao za kawaida za baishara, kilimo au
kutumia siku hiyo kupumzika kuliko kujihusisha kwenye vitendo ambavyo vinaweza
kuwaletea matatizo.
Mazoezi ya pamoja ya Vyombo
vya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera yalianzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera
na kupitia katikati ya mji wa Bukoba kuelekea Kashai na yamehitimishwa katika
Viwanja vya Gymkhana karibu na Bukoba Club.
Wito kwa wananchi wote
hususani Manispaa ya Bukoba mnakaribishwa kila Jumamosi ya kila wiki kujumuika
pamoja watumishi kufanya mazoezi ya
pamoja kwaajili kuimarisha miili yetu,
mazoezi hayo huanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa saa 12:00 Asubuhi na
kumalizikia katika viwanja vya Gymkhana
saa 3:00 asubuhi.
Post a Comment