Na: Sylvester Raphael
Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanifu wa Majengo na ujenzi
kukagua na kujiridhisha na eneo lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Kagera
kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Kisasa cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
kinachotarajiwa kujengwa kwa ufadhili wa
Serikali ya Watu china Mkoani Kagera katika Kijiji cha Burugo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Timu hiyo ya Wataalamu kutoka katika Kampuni ya ujenzi ya “China
Qiyuan
Enginering Coorparation” ikiongozwa na Bw. Fang Ke Feng walimueleza Mkuu wa Mkoa Kagera Ofisini kwake
walipofika kumsalimia kuwa wamekuja kuona eneo la chuo cha VETA kitakapojengwa
ili waweze kuchora michoro ya majengo inayoendana na eneo husika.
Baada ya kufika katika eneo la Burugo kitakapojengwa Chuo cha
VETA Mkoa wa Kagera Wataalam hao kutoka nchini China wakiongozwa na Msanifu Majengo Bw. Fang Ke
Feng waliridhishwa na eneo hilo na kusema kuwa ni eneo zuri linalofaa kwa
ujenzi na michoro wanayotarajia kuichora itaendana na eneo hilo.
“Tumeona eneo ni zuri sana, Serikali ya Mkoa imefanya kazi
yake ya kufikisha miundombinu ya umeme na barabara katika eneo la ujenzi, pia
tumeridhika na juhudi zinazoendelea kufanyika ili kuhakikisha maji yanapatikana
katika eneo hili na jambo lakufurahisha Ziwa Victoria lipo karibu sana kwa
upatikanaji wa maji katika ujenzi,” Alieleza Bw. Fang Ke Feng.
Vilevile kiongozi wa Timu hiyo ya wataalamu kutoka Nchini China
Bw. Fang Ke Feng alisema kuwa baada ya kuona eneo husika sasa itachukua muda wa
miezi miwili kabla ya ujenzi kuanza kutoka sasa ambapo watasanifu michoro ya majengo na kuiwasilisha Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia ili iidhinishwe na ujenzi utaanza mara moja.
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Stadi Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Enock Kayani alisema kuwa
ujenzi wa chuo hicho utagharimu jumla ya Shilingi bilioni 22.4 pia katika awamu
ya kwanza chuo kitadahili wanafunzi 400
na awamu ya pili wanafunzi 400 na kukamilisha jumla ya wanafunzi 800 mara baada
ya chuo hicho kuwa kimekamilika.
Pia Bw. Enock alisema kuwa tayari Serikali imeanza kuwaandaa
wakufunzi wa ufundi katika chuo cha VETA
Morogoro ili kujiandaa mapema kwaajili ya kuwafundisha wanafunzi watakaodahiliwa
katika chuo cha VETA Kagera.
Pia alisistiza kuwa Walimu hao watapelekwa nchini
china kujifunza zaidi kwani mara baada ya Chuo kukamilika kitakuwa na Mashine
za kisasa zinazohitaji ujuzi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu
akiongelea ujio wa wataalam hao kutoka nchini China alisema amefurahishwa sana
na ujio wao kwani uongozi wa mkoa na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakisubiri
kwa hamu kubwa ujenzi wa chuo hicho kuanza na Serikali ya mkoa tayari imefanya
majukumu yake ya kuhakikisha miundombinu ya umeme na barabara imefika katika
eneo husika.
Mwenyekiti wa Kiji ji Burugo
Bw. Samson K. Simon akiongea na Timu ya Wataalamu kutoaka Nchini China
Alisema kuwa imekuwa furaha kubwa kwake na wanakijiji wa Burugo kwani wamekuwa
wakisubiria kwa hamu sana ujenzi wa chuo hicho kuanza na ni matarajio yao kuwa
watapata ajira mbalimbali za kuinua vipato vyao pia ujenzi wa chuo hicho
utainua sana uchumi wa kijiji chao.
Katika hatua nyingine Timu ya Wataalamu kutoka nchini China
ilipata wasaa wa kutembela Shule ya Sekaondari Ihungo iliyopo Manispaa ya
Bukoba inayojengwa upya na Serikali ya Tanzania mara baada ya kuharibiwa vibaya
na Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016.
Lengo la Timu hiyo kufanya
ziara katika Shule ya Sekondari Ihungo ni kujionea ubora wa majengo
yanayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Post a Comment