WALENGWA wa mpango wa
kunusuru kaya masikini waliko katika mitaa ya Rubumba na Kagondo Kaifo kata za
Nyanga na Kagondo Manispaa ya Bukoba mkoani KAGERA, wameiomba serikali kupitia
mfuko wa maendeleo ya jamii(Tasaf)kuongeza kiwango cha ruzuku kwa mlengwa,lengo
ikiwa ni kufanikisha madhumuni yaliyokusudiwa ya kuhakikisha kaya masikini sana
zinaondokana na umasikini.
Rai hiyo,imetolewa na walengwa hao kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya
Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera AMATUS MSOLE wakati amewatembelea walengwa wa
mpango huo ili kujionea maendeleo ya miradi yao walioanzisha kutokana na ruzuku
wanayopokea kwa kila mwezi.
Devotha Fella mkazi wa mtaa wa Rubumba,pamoja na shukrani kwa serikali juu ya
utekelezaji wa mpango huo,ameiomba Serikali kupitia mfuko huo,kufikiria
ni jinsi gani inaweza kuongeza kiwango cha ruzuku kutoka 20,000 inayotolewa kwa
ajili ya kujikimu,kutokana na gharama za uendeshaji wa maisha kupanda na kusababisha
uwepo ugumu wa maisha.
Amesema kuwa kiwango hicho kitaongezeka,kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo
mabadiriko makubwa baina ya walengwa kutoka kwenye hali ya umasikini kufikia
hali ya kawaida ya maisha ya kati kwani mbali na kiwango kinachotolewa kwa sasa
kuwa kidogo lakini kimewezesha kusaidia kuwepo kwa mabadiriko ya maisha kwa
walengwa. .
Kwa upande wao Stella Pius na Rehema Ismail wote wakazi wa mtaa Rumumba,pamoja
na pendekezo hilo la kuongezeka kiwango cha ruzuku,pia wamebainisha kuwa ruzuku
itolewayo kwa malengo ya kupambana na umasikini,imewainua sana na kuyafanya
maisha yao yaonekane kama rahisi tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kupokea
ruzuku.
Akitoa taarifa za mpango huo,Mratibu wa Tasaf III Manispaa ya Bukoba MURISHIDI
ISSA,jumla ya shilingi milioni 153,256,500 zimetolewa na mfuko wa maendeleo ya
jamii(Tasaf) kwa ajili ya malipo ya ruzuku kwa walengwa 3,876, kiasi cha fedha
kilicholipwa wakati wa dirisha la awamu ya sita ya miezi Mei na Juni.
MURISHIDI amesema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha milioni 136,228,000
zilienda moja kwa moja kwa ajili ya ruzuku kwa walengwa,huku kiasi cha
17,028,500 ikiwa ni asilimia 1.5 inayopelekwa kwenye mitaa ili kuwezesha
shughuli mbalimbali zikiwemo za ufuatiliaji na usimamizi wa mpango huo.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa KAGERA AMATUS MSOLE amesema mbali na
kutoa pongezi kwa baadhi ya walengwa hao walioonekana kufanya mabadiriko kwa
kutumia vizuri ruzuku hiyo ya Tasaf,pia ametoa rai kwa walengwa wengine walioko
kwenye mfuko kuiga mfano kwa walengwa waliofanikiwa kwa matumizi bora ya fedha
za ruzuku.
Hata hivyo MSOLE amesema kuwa nia ya Serikali ni kuondoa watu kwenye
umasikini,hivyo baada ya miaka mitatu Serikali haitaendelea kumpatia ruzuku
masikini yeyote atakayekuwa tayari ameishapokea ruzuku kwa awamu hii,badala
yake utaratibu utakaokuwepo ni kubaini kaya nyingine zilizo masikini na
kuziingiza kwenye mpango.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment