Wananchi na wadau wa
maendeleo wilayani Karagwe mkoani Kagera wamepongezwa kwa jitihada zao za
makusudi waliozoonesha katika kuchangia suala zima la madawati, ambapo hadi
sasa kata zote za wilaya ya Karagwe zimefikisha madawati 2,324 huku halmashauri
ikiwa imeshatoa madawati 500.
Pongezi hizo zimetolewa leo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Karagwe mkoani Kagera Wailess Mashanda wakati akiongea na KARAGWE FORUM ofisini
kwake.
Mashanda amesema kuwa
wananchi na wadau wa maendeleo wilayani humu wameoonesha jitihada kubwa za
kuchangia madawati japo kufikia juni 30 mwaka huu kama agizo la Rais kuwa
wamekamilisha madawati, kwa wilaya ya Karagwe watakuwa hawajakamilisha japokuwa
wapo katika harakati za kukamilisha baada ya hapo.
Ameongeza kuwa hadi sasa
zoezi la ukusanyaji wa mbao na boriti linaendelea huku waliotoa ahadi za
kuchangia madawati nao wakiwa wanaendelea kutoa michango yao ili kuhakikisha
shule zote za wilaya ya Karagwe zinapata
madawati ya kutosha.
Hata hivyo Mashanda
amewataka wananchi ambao bado hawajachangia mchango huo wa madawati kuhakikisha
wanachangia na kufikia malengo walioyojiwekea katika vijiji,vitongoji na kata
kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Mashanda
amezungumzia kuteuliwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe
Mhandisi Richard Ruyango kuwa mkuu wa wilaya ya Muleba na kuhamishwa
kwa mkuu wa wilaya ya Karagwe Deodatus Lucas Kinawiro kuwa mkuu wa wilaya ya
Bukoba.
Post a Comment