Wananchi hao wamedai kuwa mkuu wa wilaya badala ya kutumia njia ya kukaa meza moja na uongozi wa serikali ya kijiji lakini wameshughudia vitisho vya kutumia askari na ofisi ya ardhi wilaya kutaka kufanya upimaji wa ardhi bila kushirikisha uongozi wa kijiji ambao ndiyo wenyeji wa maeneo hayo.
Diwani wa Kata ya Kihanga Rwamuhangira Steven Mgasha amesema kuwa kuna dhana inapitishwa kuwa wananchi wa kihanga hawapendi ujenzi wa chuo kikuu ameongeza kuwa hiyo inatumika kupoteza hali halisi ilivyo kwani na wao wanahitaji maendeleo na pia ujirani mwema ila wanachohitaji na utaratibu wa kutoonea mtu na maendeleo yawe ya wote.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kishoju Dawson Bampabula amesema serikali ya kijiji inashindwa kuendesha shughuli zao kwa uhakika kutokana na vitisho vinavyotolewa na mkuu wa wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro hadi kufikia kuwaweka ndani kwa madai kuwa wao ndiyo wanachochea mgogoro pia kwa kile alichoeleza kuwa walishindwa kutekeleza agizo la kugawa ardhi wakati wao hakuna mwananchi ambaye walishawahi kumnyanganya ardhi.
Mkuu wa wilaya ya Karagwe alipofuatwa na waandishi wa habari kujibu madai hayo ya wananchi amejibu kwa ufupi na kuatia maelezo kuwa mgogoro huo ameisha umaliza na tayari amefunga mjadala huo na kuongeza kuwa Dayosisi ya KKKT Karagwe wanamiliki kihalali.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Dayosisi ya KKKT Karagwe Mchungaji Anaceth Magayane akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa dayosisi hiyo inamiliki ardhi hiyo kihalali na walipewa mwaka 1980
Post a Comment