Wanachama na mashabiki wa Yanga, usiku huu wametua
nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa
Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili ya
matibabu.
Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro na walimkabidhi Manara kiasi ya Sh 1,055,000
kama mchango wao.
Wiki iliyopita, Manara aliamka jicho la kushoto halioni.
Pia jicho lake la kushoto halioni vizuri pia. Hivyo anatarajiwa
kupelekwa India kwa ajili ya matibabu na safari yake
huenda ikawa Jumamosi hii.
Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi
mbalimbali ya mitandao ya Wanayanga.
“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni
mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.
“Nyie sasa mmredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao
walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba, Yanga wanazika Simba.
Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema.
Post a Comment