Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na
maeneo ya hifadhi kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza
maeneo hayo bila kuondoa ushiriki wa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
Kauli hiyo ameitoa katika mafunzo
yaliyoandaliwa na Shirika hilo kwa wadau
wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, yaliyofanyika
katika hoteli ya Kilimanjaro Resort kufuatia makubaliano na serikali ya
Tanzania.
Akizungumza na washiriki amesema
kuwa UNESCO inachofanya ni kuanzisha safari ambayo inaweza kuwa ngumu na ndefu
lakini washiriki wake ni lazima kutambua namna ya kuendelea kufanya menejimenti
ya maeneo ya hifadhi na urithi wa dunia kwa manufaa ya kizazi cha sasa na
kijacho
Akifungua mafunzo hayo ambayo
wataalamu ni washiriki wenyewe wakitumia njia ya kuelewa ya methodolojia ya
uchambuzi wa vikwazo (Bottleneck Analysis Methodology) amesema safari ya
kufanikisha menejimenti ya maeneo hayo duniani na hasa hapa nchini Tanzania ni yenye changamoto nyingi na kwamba
wadau wote wanatakiwa kuwa pamoja kuvishinda vikwazo hivyo na kuifanikisha
safari yao.
Rodrigues akizungumza katika Warsha hiyo ambayo imechukua wadau mbalimbali
wa masuala ya urithi na menejimenti zake kutoka serikalini, taasisi zisizo za
kiserikali na wananchi wengine, amesema kwamba maeneo hayo yamezungukwa na
wananchi na pamoja na kuwawekea sheria za kutoharibu na kuyachakaza ipo haja ya
kushirikiana nao namna ya kupanga kuyaendeleza maeneo hayo huku yakiwa yamebaki
katika hali inayotakiwa.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea
uwezo wa kupanga maendeleo katika maeneo ambayo ni ya urithi wa dunia, binadamu
na maeneo ambayo uhai unaweza kuwepo.
Aidha akifafanua zaidi amesema
mafunzo hayo yamelenga kuwapa wahusika nadharia zinazofaa katika safari ndefu
ambayo UNESCO nayo itashiriki na isingelipenda kumwacha hata mtu mmoja nyuma.
Mafunzo hayo yanatolewa kufuatia
mpango wa UNESCO wa kutaka kuwa na uhakika na kuhami maeneo hayo ya urithi;
huku mamlaka zikitoa ushirikiano ili kuwezesha malengo ya maendeleo endelevu,
ambayo ndiyo ajenda ya dunia kuelekea 2030, yanafikiwa bila kuathiri maeneo
tajwa
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Related Posts
- KAGERA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUENDELEA KUJIIMARISHA KUWALINDA RAIA NA MALI ZAO25 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Vyombo ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera vyafanya mazoezi ya ...Read more »
- MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA ZA KARAGWE NA NGARA PIA HITIMISHO WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mwenge wa Uhuru waendelea kuchanja mbuga Mkoani Kagera kwa ku...Read more »
- MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI KAGERA NA KUANZA UZINDUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA ZAIDI YABILIONI 1216 Apr 20180
Na: Sylvester Rapahel Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo April 8, 2018 Mkoani Kagera na...Read more »
- TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA16 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Serikali ya Watu wa China yatuma timu ya Wataalam wa Usanif...Read more »
- MKOA WA KAGERA WAVUKA LENGO KATIKA UNDIKISHAJI WA WANAFUNZI AWALI NA DARASA LA KWANZA MWAKA 201816 Apr 20180
Na: Sylvester Raphael Mkoa wa Kagera wavuka lengo la uandikishaji wa Wananfunzi katika madarasa...Read more »
- MKUU WA MKOA KAGERA AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUFIKISHWA OFISINI KWAKE AKIWA NA PINGU MIKONONI BAADA YA KUITIA SERIKALI HASARA08 Mar 20180
Na Sylvester Raphael Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampun...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.