Wananchi wilayani Karagwe
mkoani Kagera wamewaomba viongozi wao waliowachangua kuangalia kwa karibu suala
la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao kwani ni moja wapo ya
ahadi walizohaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wakiongea na kituo hiki
baadhi ya wananchi wa wilaya ya Karagwe wamesema kuwa katika maeneo yao kuna
tatizo kubwa la kufuata maji kwa umbali mrefu na maji hayo siyo safi na salama
kwa matumizi ya kila siku ya binadamu.
Wamesema kuwa wakati
viongozi wao wanagombea nafasi za uongozi walihaidi kuwapatia maji ,hivyo
kuwaomba kutekeleza ahadi hiyo kwani ukosefu wa maji unawasababishia wananchi
kutoshiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwani wakati mwingine
wanafuata maji siku nzima .
Diwani wa kata ya
Nyakahanga Charles Bechumira ambaye amekiri kuwepo kwa tatizo la maji katika kata ya Nyakahanga huku
akiwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati suala hili likifanyiwa kazi na
viongozi wa ngazi husika.
Kwa upande wake mbunge wa
jimbo la Karagwe Innosent Bashungwa ameeleza kuwa anaendelea kufanya jitihada za makusudi ili
kutumiza ahadi yake aliyohaidi wananchi wa wilaya ya Karagwe kuhusu kuwasogezea
maji karibu huku akieeleza juu ya kuanza kwa mradi mkubwa wa maji utakaosambaza
maji wilaya ya Karagwe kutoka katika ziwa Rwakajunju.
Post a Comment