Wamiliki wa
baa na vilabu
vya pombe wilayani
Karagwe wametakiwa kutotumia au kuuza
pombe kwa saa
za kazi hadi
majira ya saa
kumi jioni ili
kutii sheria inavyoelekeza
na atakayeenda kinyume
na utaratibu huo
atachukuliwa hatua za
kisheria kwa kuikosea
jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Kauli hiyo
ilibuka katika mkutano wa
kutoa elimu kwa
walengwa wa mpango
wa TASAF 111 uliofanyika hivi
karibuni kwenye ofisi
ya kijiji cha Kanoni kata
ya Kanoni wilayani
Karagwe mkoani Kagera Mwenyekiti wa
kamati ya Elimu,Afya na
maji Charles Bechumila
akihamasisha walengwa kujiunga
na mfuko wa
afya ya jamii
yaani CHF amesema amechukizwa
na kitendo cha
baadhi ya wananchi
wa stesheni ya
Rwambaizi kuonekana wakichoma
nyama na kunywa
pombe saa za
asubuhi ambazo ni
za kazi.
Amesema huwezi
kuondokana na umaskini
bila kuwa na
matumizi sahihi juu
ya kupata na
kutumia pia ameongeza
kuwa lazima kuwa
na afya ndipo
utapata nguvu za
uzalishaji hivyo akawataka
walengwa hao kujiunga
na mfuko wa CHF
kwa kuchangia shilingi 15000 kwa mwaka na
watatibiwa bure watu
sita kwa mwaka huo
wote.
Kutokana na
kauli hiyo ya
unywaji pombe saa
za asubuhi mwenyekiti
wa halmashauri ya
wilaya ya Karagwe
Wallesi Mashanda akatoa
kauli kwa watendaji
na kuwataka kujisimamia
na kutekeleza sheria
kukomesha tabia hiyo.
Hata hivyo
amesema siku nyingine
akiwa kwenye ziara
ya kukagua shughuli za
maendeleo akikutana na
hali hiyo ya
unywaji wa pombe
saa za kazi
hataivumilia.
Post a Comment