MOROGORO
PRESS CLUB (MOROPC)
Chairperson:
Nickson Mkilanya
+255713200018
Executive
Secretary: John Kidasi
+255653912959
Treasurer:
Merina Robert
+255782467274
Coordinator:Thadei
Hafigwa
+255754683186
E-mail:moropc97@gmail
com.
P.O.Box 1462, MOROGORO
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KWA
NIABA YA UONGOZI WA MOROGORO PRESS CLUB NA WANACHAMA WAKE, TUNAYOFURAHA KUBWA
YA KUWAPONGEZA WANACHAMA WAKE WALIOTEULIWA HIVI KARIBUNI NA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, DK.JOHN POMBE MAGUFULI KUSHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA
UTUMISHI WA UMMA.
NDUGU,
SIMON SALES BEREGE, KASILDA MLIMILA NA ZABRON BUGINGO NI WANACHAMA WETU WA
KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MOROGORO NA BAADHI YAO WALIWAHI KUSHIKA
NAFASI ZA UONGOZI WA KLABU YETU KWA NYAKATI TOFAUTI.
SIMON
SALES BEREGE AMETEULIWA KUWA
MKURUGENZI,HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA –SHINYANGA,AKIWA MKOANI
MOROGORO ALIHUDUMU NAFASI YA NAIBU KATIBU MKUU WA MOROGORO PRESS CLUB,NAFASI
HII ALIITENDEA HAKI KWA KUIFANYA KWA UFANISI MKUBWA.
PIA
KASILDA MGENI MLIMILA AMETEULIWA KUWA KATIBU TAWALA WILAYA YA BAHI,DODOMA
ALIWAHI KUHUDUMU NAFASI YA UHAZINI WA MOROGORO PRESS CLUB,AMBAPO MWAKA JANA
KAMATI TENDAJI YA MOROGORO PRESS CLUB
ILIMTEUA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA MIPANGO,UCHUMI NA FEDHA
ANAYEIHUDUMU HADI SASA.
BW.ZABRON
BUGINGO AMETEULIWA KUWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWALICHA YA
KUWA MWANACHAMA HAI WA KLABU YETU DAIMA AMEKUWA NI MSHAURI MKUBWA KATIKA
MASUALA YA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANAHABARI WA MKOA WA MOROGORO, WOTE KWA
PAMOJA TUNAWAPA PONGEZI KUBWA KWA KUAMINIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO CHINI
YA DK.MAGUFULI, NI IMANI YA KUWA WATAKUWA WATUMISHI WAADILIFU, WACHAPAKAZI KWA
MASILAHI YA UMMA.
KWETU
SISI MOROGORO PRESS CLUB, TUNAONA NI UFAHARI KWETU KWA KUTOA WATU WENYE
UADILIFU NA KUAMINIKA KWA UMMA WA TANZANIA NA SERIKALI KWA UJUMLA WAKE.
KWANI
KWA SIKU ZA HIVI KARIBUNI TUMEWEZA KUTOA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA TIKETI
YA CHADEMA, DEVOTHA MINJA.
PIA
WAPO WANACHAMA WETU WENGINE WA MOROGORO
PRESS CLUB WALIWEZA KUAMINIKA KWA KUCHAGULIWA
KATIKA NAFASI ZA UDIWANI,SAMUEL MSUYA AMBAYE NI DIWANI WA KATA YA
MBUYUNI (CCM) NA LATIFA GANZEL DIWANI WA VITI MAALUM CCM.
WOTE
HAO NI MATUNDA YA MOROGORO PRESS CLUB,TUNAAMINI YA KUWA KLABU YETU KUTOKANA NA KUWA NA WANACHAMA WENYE
ELIMU,UJUZI,MAARIFA NA UADILIFU WENYE TIJA KATIKA JAMII WATAPATA NAFASI YA KUWAHUDUMIA
UMMA WA TANZANIA KATIKA NAFASI MBALIMBALI KWENYE TAASISI NYINGINE NJE YA MOROGORO PRESS CLUB
IKIWEMO SERIKALINI.
SISI
MOROGORO PRESS CLUB,WANACHAMA WETU WOTE WALITEULIWA NA KUSHIKA NAFASI ZA
UONGOZI NI WATU MAKINI NA WENYE UADILIFU MKUBWA,HIVYO TUNAWATAKIA UTUMISHI
MWEMA WATAENDELEZA NA UADILIFU WAO KATIKA NAFASI ZA UTUMISHI KATIKA MAENEO
WALIOPANGIWA KUTOA HUDUMA,TUNAWASIHI WAENDELEE KUWA MABALOZI WA MOROGORO PRESS
CLUB.
IMETOLEWA
NA
…………………………..
NICKSON
MKILANYA
MWENYEKITI,
MOROGORO PRESS CLUB
8/7/2016
Post a Comment