Watendaji wa
vijiji na Kata
wametakiwa kuzungukia maeneo
ambayo wanafanyia kazi
ili kubaini baadhi
ya wakulima wa
Kahawa wanaokiuka agizo
la serikali la
kutovuna kahawa mbichi
na kuzianika chini
waweze kuchukuliwa hatua
za kisheria dhidi
yao.
Agizo hilo
likmetolewa na mwenyekiti
wa halmashauri ya
wilaya ya Karagwe Wallesi Mashanda
baada ya kukuta
mkulima wa kahawa
Filidolini Nestory wa
kitongoji cha Omukilama kijiji
cha Kanoni kata
ya Kanoni wilaya
ya Karagwe amevuna
kahawa mbichi kitendo
ambacho kimeelezwa ni
kuikosea Jamhuri na
baadhi ya wakulima
wanaofuata masharti
yaliyowekwa na serikali.
Amesema kutokana
na hali hiyo
kujitokeza watakuwa wanafanya
ziara za kushtukiza
ili kuwabaini wanaovuna kahawa
mbichi na kuwachukulia
hatua kali dhidi
yao .
Kufuatia hali
hiyo Walles Mashanda
ametoa agizo kwa
mtendaji wa kijiji
cha Kanoni Peter
Rwabishengo kuwatafuta wanamgambo
kuhakikisha kahawa hizo
mbichi zinazolewa na
kuteketezwa ambapo wanangambo
watatu Agustine Elias,Majaliwa Edward
na Philimoni Rugarabamu
wakaanza kutekeleza agizo
hilo.
Hata hivyp
mkulima Revelian Kamuhangile
ambaye amekutwa akianika
kahawa zao amepongezwa
na kamati hiyo
kwa kuanika kahawa
vizuri na zilizoiva.
Post a Comment