Ili
maonesho ya siku kuu ya wakulima
maarufu Nane Nane yaweze kufanyika ngazi
ya Wilaya inategemea uwezo na Bajeti ya
Halmashauri husika.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Kilimo wa
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Cleophace Kanjagaile wakati akijibu hoja za
wananchi kupitia vyombo vya habari waliomba maonesho hayo yaweze kufanyika katika
ngazi ya Wilaya ili kuwawezesha wakulima
kushiriki kwa wingi na kupunguza gharama za wao kushiriki maonesho hayo ngazi ya mkoa.
Amesema
miaka 4 imepita bila maonesho hayo kufanyika ambayo yalikuwa yakifanyika kwa ngazi ya wilaya katika kata mbalimbali za wilaya
hii na kwamba hayafanyiki kutokana
na kuwa kila halimashauri ni lazima kushiriki maonesho ya Kikanda
ambayo hufanyika Mwanza kanda ya ziwa na
mkoa katika Manispaa ya Bukoba
Viwanja vya Kyakailabwa na ikifanyika
kwa ngazi ya
wilaya zinahitajika shilingi
million 100 ili kufanikisha maonesho hayo.
…………………………Insert………………
Amesema
kama Idara ya kilimo wana wanatambua
umuhimu kusogeza maonesho haya Karibu na
wa wakulima kwani ndio walengwa wakuu
lakini wanalemewa kufuatia kuwa maonesho ya Kikanda na mkoa ni ya lazima.
Ametoa
wito kwa wadau wa kilimo na maendeleo, Taasisi zakifedha na makampuni
mengine kushiriki kwa pamoja na
kuwezesha kufanikisha maonesho hayo endapo watafuatwa pale yatakapofanyika kwa ngazi ya
wilaya ili kuwawezesha wakulima wasio na uwezo wa kuchangia kushiriki
kikamilifu siku yao.
Post a Comment