Wananchi katika mamlaka ya mji
mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuchangamkia fursa
ya kupima viwanja vyao ili kuepuka migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima
inayojitokeza mara kwa mara.
Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa Kampuni ya Mataro Land developers
Tanzania Limeted iliyoko jiji Mwanza
inayojihusisha na upimaji wa ardhi Joeli
Mataro
Mataro amesema kuwa kuna faida nyingi za kupima kiwanja mojawapo ikiwa ni
kuepuka migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima ambayo imekuwa ikijitokeza katika
sehemu mbalimbali hapa Tanzania.
Mataro ametaja taratibu ambazo mwananchi anatakiwa kuzifuata endapo
ataamua kupima kiwanja chake huku akieleza kuwa hadi sasa gharama za upimaji wa
viwanja zimepungua na kufikia kiasi cha shilling laki mbili ambayo kila
mwananchi na uwezo wa kuipata.
Post a Comment