Mkuu wa
wilaya ya Karagwe
Godfrey Muheluka amewataka
wananchi wilayani Karagwe
kuhakikisha maeneo yao
yote yanakuwa safi
wakati wote na
kesho Alhamisi itakuwa
ni siku maalumu
ya uzinduzi wa
ukaguzi wa usafi wa
mazingira.
Ametoa agizo
hilo leo katika
kikao cha kamati ya
Huduma za Afya
ya Msingi PHC wilaya
ya Karagwe kilichofanyika katika
ukumbi wa ofisi
ya mkuu wa
wilaya ya Karagwe baada
ya kupewa taarifa ya
kusuasua kwa hali
ya ushiriki wa
wananchi kufanya usafi.
Muheluka amesema
kuwa utaratibu wa kufanya
usafi unafahamika hivyo
kinachotakiwa ni kukagua
maeneo yote na
kuwataka viongozi kuanzia
ngazi ya vitongoji
hadi wilaya kuhakikisha
maeneo yote yanakuwa
safi wakati wote.
Amesema kwa
siku ya Kesho
Agosti 11 shughuli zote hatafanyika
kuanzia saa moja
hadi saa nne
asubuhi itakuwa ni
usafi hivyo huduma
za ofisi na
maeneo ya biashara
zitaanza saa nne
hivyo watu wote
wakashiriki usafi na atakayekutwa
eneo lake ni
chafu faini yake
ni shilingi laki
moja au kifungo cha
miezi sita au
vyote kwa pamoja.
Hata hivyo
amewataka wajumbe wa kamati ya
Huduma za Afya
ya Msingi PHC wilaya
ya Karagwe kuripoti
ofisini kwake bila
kukosa ili zoezi
la ukaguzi liweze
kuanza mara moja.
Post a Comment