Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza
katika Kata Nyakibimbili Kijijini Kitahya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Agosti 9, 2016 katika chanzo cha maji
kilichopo kijijini hapo ili kuhakiki kama pampu ya kusukuma maji kama ilifungwa na ipo katika tenki la maji
lilojengwa katika chanzo hicho cha maji.
Mkuu huyo wa Wilaya aliamua
kufanya ziara hiyo ya ghafla na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama mara baada ya
kuletewa malalamiko na wananchi kuwa siku mradi huo ulipowekewa jiwe la msingi
na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima Julai 27, 2016 maji
yaliyotoka katika ghati la Ibwera yalijazwa kwenye tenki na gari la kubebea
maji kwani pampu ya kusukuma maji
haikuwepo katika tenki lilipo kwenye chanzo cha maji.
Baada ya kufika katika
chanzo hicho cha maji Kinawilo aliyeongozana pia na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Gregory Fabian, Mhandisi wa Maji Dismas Martin, na Mhandisi Mshauri wa Mradi
huo Mwesiagwa Mtagaywa wa Kampuni ya (O & A Company Ltd.) alikagua mradi
huo na kugundua kuwa pampu ipo na inafanya kazi vizuri ya kusukuma maji.
Aidha, iligundundulika kuwa
maji mara baada ya kusukumwa kutoka
kwenye tenki umbali wa mita 22 kutoka
kwenye tenki hilo bomba limekatika kiungio jambo linalosababisha maji kutopanda
hadi katika Kata ya Ibwera ambapo Mhe. Kinawilo alimuagiza Mhandisi Mshauri
kuhakikisha anamshauri Mkandarasi kufanya marekebisho ya haraka nadani ya wiki
moja.
Aidha , katika mradi huo
kuliibuliwa suala la wananchi kukata mabomba ya maji katika chanzo hicho na
kusababisha maji kutoenda katika tenki linalohudumia vijiji vitatu vya Kitahya,
Kibona na Itongo na kusababisha Diwani wa Kata ya Nyakimbimbili Haji Matsawilly
Juma kulalamika kuwa maji hayawafikii wananchi na kumwomba Mkuu wa Wilaya
kumhimiza Mkandarasi kumaliza kazi ili maji yatoke kwa wananchi kama
ilivyotarajiwa.
Maagizo, Kinawilo baada ya kushuhudia uharibifu huo
alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anafunga vifaa vyenye ubora
ili thamani ya vifaa iendane na gharama za mraddi huo. Pili alimwagiza
Mwenyekiti wa Kijiji Kitaya
Bw.Johnstone Kahigwa aliyedai kuwa kijiji hakikukishirikishwa tangu
mwanzo wa mradi kuhakikisha anashirikiana na Halmashauri ya kijiji chake
kuilinda miundombinu ya mradi huo kwa sababu mradi upo katika eneo lake.
Vilevile Kinawilo alimwagiza Mhandisi Mshauri
kuhikikisha anfanya marekebisho yote ya mradi huo ndani ya wiki moja ili
wananchi waanze kupata huduma ya maji. Na mwisho aliwaagiza Watendaji wa Kata
za Ibwera na Nyakibimbili kuititsha mkutabno wa pamoja kwa kamati za maji za Vijiji
vya Kitaya, Kibona,Itongo na Ibwera ili kuweka mikakati ya kuilinda miundombinu
ya mradi huo wa maji.
Mradi huo wa maji
ukikamilika unatarajiwa kuhudumia vijiji vinne vya Kitaya, Kibona,Itongo (Kata Nyakibimbili)na Ibwera (kata Ibwera)
una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 430 na ulianza katika awamu ya kwanza
mwaka 2009 katika upembuzi yakinifu na usanifu, aidha utekelezwaji wake ulianza
rasmi katika awamu ya pili iliyoanza
Mwezi Julai, 2013.
Post a Comment