Zikiwa zimebaki siku
chachee kuazimisha siku ya kunyonyesha duniani wanawake wilayani Missenyi
wameshauriwa kula mlo kamili pamoja na kunywa maji mengi katika kipindi cha
mimba.
Afisa lishe wilayani MISSENYI ZAINATI JAWADU ametoa kauli hiyo wakati akiongea
na vyombo vya habari juu ya wito kwa wanawake wote kabla ya kuadhimisha siku ya
unyonyeshaji.
ZAINATHI amesema kuwa mlo kamili kipindi cha mimba ni matokeo ya kuzaa mtoto
mwenye afya pamoja na kupunguza magonjwa mbalimbali pale mtoto
anapozaliwa.
Akiongelea kipindi mtoto anapozaliwa amesema kuwa maziwa ya kwanza baada ya saa
moja kujifungua ni maziwa muhimu na yana virutubisho ambavyo uwezi kuvipata
katika maziwa yeyote.
Aidha amewataka wanawake kujiamini pindi wanapojifungua kuwa wanauwezo wa
kuwanyonyesha watoto wao bila maziwa kupotea mpaka miezi sita huku akiwataka
wanawake waliojiriwa kuacha tabia ya kuwaacha watoto wachanga muda mrefu bila
kuwanyonyesha
..
Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi walezi kuwapa watoto wadogo samaki ambapo
amesema kuwa mafuta yanayopatikana kwenye samaki hayawezi kupatikana katika
kitoweo chochote.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment