Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa Mkoani Kagera katika siku yake ya
pili mara baada ya siku ya kwanza kuitumia kutatua migogoro ya wananchi kuhusu
ardhi siku ya pili ya tarehe 19.08.2016 aliitumia kuaongea na watendaji mbalimbali wa Serikali akiwa mkoani hapa.
Eneo
la kwanza aliloliongelea Mhe. Lukuvi ni kuhusu migogoro ya ardhi
kwa wanachi iliyo mingi ilisababishwa na
Watendaji wa Serikali waliopewa dhamana ya kushughulikia suala la ardhi, ambapo
aliwaonya Watendaji wote kuacha tabia hiyo mara moja. Agizo, aliwaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa wote nchini kuwachukulia
hatua za kinidhamu au kuwafukuza kazi Watendaji
hasa Maafisa Ardhi watakobainika kusababisha migogoro ya ardhi katika maeneo
yao.
Katika Agizo hilo Mhe.
Lukuvi alimpa Onyo kali Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw.
Projestus Katabalo kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea bila kufuata
sheria, taratibu na kanuni za utekelezaji wa zoaezi la uthamini.
Eneo
la pili, Mhe. Lukuvi alisema kuwa kupitia Wizara yake Serikali
imepanga ndani ya miaka kumi kuwa itakuwa imepanga, imepima na kumilikisha
ardhi yote ya Taifa la Tanzania. Agizo,
Mhe. Lukuvi aliagiza Mikoa yote nchini kuanza kuweka mipango ya kupanga, kupima
na kumilikisha ardhi. Aidha aliuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha
unatoa hati miliki elfu kumi za ardhi kwa mwaka huu wa fedha 2016/17ambapo
lengo la kitaifa ni hati Laki nne.
Agizo la
pili ni kuhusu kupima maeneo yote ya Serikali (Serikali za Mitaa na Serikali Kuu)
pamoja na kubaini majengo yote ya Serikali ambapo yeye kama Waziri mwenye
dhamana atatoa hati maalum yenye msamaha wa kodi ya kumiliki maeneo ya Serikali
ili yaachwe bila kuingiliwa na wananchi.
Agizo la
tatu, ni Maafisa Mipango Miji kuhakikisha wanaainisha maeneo yote yaliyoiva
kuwa miji ili yapangwe, kupimwa na kumilikishwa kwa hati za muda mrefu badala
ya hati za kimila. Agizo la nne ni
maeneo yote ambayo wananchi walijenga miaka ya zamani na yapo katika miji
(Makazi Holela) nyumba zisivunjwe bali wananchi Warasmishiwe makazi hayo kwa
kuyapanga.
Eneo
la Tatu aliloongelea Mhe. Lukuvi ni Kuhusu Migogoro Mikubwa ambapo alisema kuwa katika migogoro hiyo
mfano wakulima na wafugaji, alisema kuwa Serikali imeamua kuunda kamati ya Wizara
nne ili kamati hiyo ipitie migogoro yote mikubwa na kutoa ushauri kwa Mawaziri wa Wizara hizo
husika ili kukomesha kabisa migogoro hiyo.
Wizara hizo nia Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo,
TAMISEMI, na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Angalizo
mikoa yote iliagizwa kuacha ugawaji wa Kata na Vijiji wakati wa Uchaguzi Mkuu
bila kuihusisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwani mipaka
inayotolewa na Mikoa inashindikana kuonana na mipaka ambayohupimwa ardhini na Wizara ya Ardhi. Ili kusuluhisha
hilo aliagiza Wizara yake kupewa taarifa pale Mikoa inapotaka kugawa maeneo
yake lakini kwa sababu za msingi bila shinikizo la wanasiasa.
Katika kuhitimisha Mhe.
Lukuvi alisema kuwa Wizara yake inatengeneza sera ya Ardhi, Nyumba na Makazi
ambaop aliagiza Maafisa Mipango Miji wote nchini katika Halmashauri, Miji,
Majiji, na Manispaa kuhakikisha wanaitisha vikao vya wadau ili kuamua aina ya
rangi zipakwe katika miji badala ya kila nyumba kupakwa rangi yake na lengo ni
kuifanya miji ipendeze kwa kuwa na mpangilio wa upakaji wa rangi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu alimshukuru Mhe. Lukuvi kwa kufanya ziara
yake Mkoani Kagera na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo alimuhaidi
Mhe. Lukuvi kuwa maelekezoa na maagizo
yake yote yatafanyiwa kazi na wahusika
ili kuhakikisha migogoro ya ardhi inakomeshwa Mkoani Kagera.
Post a Comment