Kamati ya
Amani na Maadili
ya wilaya ya
Karagwe mkoani Kagera
inayoundwa na viongozi
wa dini kutoka
madhebu mbalimbali ya
kikristo na uislamu
imewataka wananchi wa wilaya
ya Karagwe kutunza
na kudumisha amani iliyopo ili isipotee
kwani ikipotea kuirudisha
siyo rahisi.
Wametoa kauli
hiyo katika kikao
chao cha pamoja
na mkuu wa
wilaya ya Karagwe
Godfrey Mheluka kilichofanyika kwenye
ukumbi wa ofisi
ya mkuu wa
wilaya ya Karagwe.
Viongozi hao
wamesema amani iliyopo
inabidi kutunzwa kwa
gharama yoyote ile
kwani ikipotea kuirudisha siyo
rahisi kama ambavyo
baadhi ya watu
wanataka kuichezea amani
iliyopo hivyo wakawataka
wananchi pamoja na waumini
wao.
Askofu wa
jimbo Katoliki la
Kayanga Almachius Vicent
Rweyongeza ambaye ni
mlezi wa kamati
hiyo ya Amani
na Maadili amesema
wao viongozi wa
kiroho wanazo kazi
tatu kwenye wito
waliokubali kuutumikia ambapo
anabainisha hapa.
Amesema katika
kutumikia Mungu awategemei
malipo lakini Mungu
mwenyewe huwalipa kazi
hiyo kwa kuwapatia
afya njema hivyo
kumtambua ni muhimu
na amesema maandamano yoyote
hayawezi kuleta tija
kama mtu au
watu hawataweza kufanya
kazi kwa pamoja.
Katibu wa kamati
ya Amani na
Maadili Mdashiru Kalokora
ambaye pia ni
katibu wa Baraza
la Waislamu Tanzania
BAKWATA wilaya ya
Karagwe na Kyerwa
amesema kamati hiyo
imekamilika na imezingatia uwiano sawa
hivyo akawataka wananchi
kuipa ushirikiano.
Makamu mwenyekiti
wa Kamati hiyo
ya Amani na
Maadili naye pia
ameweza kusema kuwa
utii wa mamlaka
kwa kufuata misingi
iliyowekwa itasaidia kudumisha
amani na kuongeza
kuwa kitu kikiwepo watu
hawaezi kuona umuhimu
wake lakini kikiondoka
ndiyo hutambua hilo
hivyo akawasihi wananchi kutothubutu kuipoteza Amani.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya
ya Karagwe amewahakikishia wajumbe
wa kamati hiyo
kuwa watakuwa ni
sehemu ya kamati
ya ulinzi na
usalama ya wilaya
na kuongeza kuwa
watakayojadili na kufikia
uamuzi watayaheshimu.
Post a Comment