Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Meja Jenerali Salum M.Kijuu katika kuteleza agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe
29/04/2009 linalomtaka kuzisimamia Halmashauri za Wilaya kila moja kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo,
Mkuu wa Mkoa tayari ameagiza kuchukuliwa
hatua kwa watendaji 8 waliohusika na uzembe na upotevu wa fedha za Serikali
katika Halmashauri mbili za Wilaya alizopitia kusimamia zoezi hilo.
Mhe. Kijuu tayari amesimamia
zoezi la kujadili Taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Halmashauri
za Wilaya ya Bukoba Muleba na Ngara ambapo katika zoezi hilo aliagiza hatua kuchukuliwa mara moja kwa
Watendaji saba Katika Halmashauri ya
Wilaya ya Bukoba na Mtendaji mmoja katika
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Katika Halmashauri ya Wilaya
ya Bukoba Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2015 ilibainisha
hoja zenye tafsiri ya kuwepo Ubadhirifu, wizi na Uzembe pamoja na ukiukaji wa
makusudi wa sheria za fedha na sheria za manunuzi ambapo watumishi wafuatao
walihusika nao ni kama ifuatavyo:
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
(Bi Grace Uyabange), Mfamasia wa Halmashauri (Bw. Edward Kabandami), Mganga
Mkuu wa Wilaya aliyehamia Katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba (Dk. Hamza
Mgula) ambapo Katibu Tawala wa Mkoa aliagizwa Kumrejesha kujibu Hoja
zinazomkabiri. Wengine ni Afisa Elimu Sekondari (Bw. Lucas Mzungu), Afisa
Utumishi (Bw. Maginga Mang’oa), Mhasibu Mapato ya Ndani (Bw. Aristides
Rwegoshora) na Mweka Hazina (Bw. Jonathan Katunzi)
Watumishi waliotajwa
walihusika kufanya yafuatayo kila mmoja kulingana na nafasi aliyokuwepo kama
msimamizi mkuu wa eneo hilo, Kwanza
ni kufanya Mabadiliko ya mkataba wa
Ujenzi wa kituo cha Mabasi (Bus Stand) ya Kemondo (Tshs 44 milion) bila idhini
ya Bodi ya zabuni ya Halmashauri kinyume
na Kanuni za Manunuzi kanuni ya 110 (5).
Pili, kulipa Mishahara
kiasi cha Tshs 28,072,549/= iliyolipwa
kwa Watumishi hewa (watoro na waliostaafu ) wakiwemo watumishi wa idara ya Elimu Sekondari ambapo, kutokana
na uzembe wa Afisa Elimu Sekondari Wilaya na Afisa Utumishi wa Wilaya
(2014/2015) kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kukagua na kuchukua hatua za
kuwaondoa watumishi wasiostahili kulipwa kwa wakati katika orodha ya malipo (Payroll),
walisababisha Serikali kupata hasara ya Tshs 28,072,549/= na kuzilipa taasisi
mbalimbali za fedha makato hewa ya kisheria kiasi cha Tshs 9,811,947.55
Tatu, Kubadili matumizi ya
fedha za ujenzi wa daraja la Kyamabale kiasi cha Tshs 200,000,000/= bila
kuzingatiwa taratibu za kubadili matumizi ya fedha za maendeleo na kusababisha
kutokamilika hadi sasa, ujenzi wa daraja lililolengwa kuondoa kero kwa wananchi
halijakamilika na lilitakiwa kukamilika tarehe 26 Oktoba, 2015. Nne, Manunuzi ya vifaa tiba na madawa
ya Hospitali Tshs 16,339,050/= kufanyika
bila dihini ya Bodi ya zabuni 2009/2010. Hoja hiyo ilitokana na baadhi
ya watumishi kutoheshimu sheria na miongozo ya Serikali kwa kisingizio cha
dharura.
Tano, Manunuzi ya mafuta
ya thamani ya Tshs 12,789,364 (mwaka 2013/14) ambayo kwa sasa ni sawa na lita
6,394 ambayo yangewezesha gari moja kusafiri umbali wa kilometa 31,973. Mafuta
hayo pamoja na kulipiwa na Halmashauri, hakuna uthibitisho kuwa yalipokelewa
katika vitabu vya kupokea mali za Halmashauri na hakuna udhitisho wa matumizi
yake. Haya ni manunuzi hewa.
Sita, Kesi za mapato ya
Halmashauri zilizokwishatolewa maamuzi na Mahakama na ilipaswa kutekeleza
hukumu kupitia Mwanasheria wa Halmashauri. Zaidi ya Tshs 14,800,000/= za
Halmashauri hazijafuatiliwa kwa kutekelezwa ama kukaza hukumu na mwanasheria wa
Halmashauri. Saba, Matumizi ya Tshs
7,150,000/= za mapato ya ndani bila kufuata taratibu za fedha na hakuna nyaraka
zozote zilizoidhinisha na kuthibitisha
matumizi ya fedha hizi ambazo zilipokelewa na mtunza fedha.
Mwisho, Ujenzi
wa ofisi ya Afisa Elimu (Sekondari) Tshs 59,500,000/=. Ofisi hii imekamilika
lakini haitumiki kwa sababu fedha zote
zilitolewa na Serikali lakini Mkandarasi
hajalipwa. Hii inaongeza deni la Halmashauri kwa mujibu wa mikataba kwa sababu
fedha zilibadilishwa matumizi bila idhini ya Mamlaka.
“Kutokana
na ukiukaji wa sheria za usimamizi wa watumishi, udhaifu katika usimamizi wa
fedha na manunuzi, Mkurugenzi na Baraza la Madiwani wachukue hatua za kinidhamu
mara moja na kuniletea taarifa ya utekelezaji wa agizo langu ifikapo tarehe 30
Agosti, 2016.” Aliagiza Mhe. Kijuu
HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA
Mhe. Kijuu alimwagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngara Bw. Aidan J. Bahama na Baraza la
Madiwani kuchumchukulia hatua za kinidhamu Afisa Manunuzi wa Halmashauri Bi
Perpetua Rulimbike ikiwa ni pamoja na kumuondoa katika kitengo cha manunuzi kwa
kusababisha upotevu wa Shilingi Milioni 24,000,000/= za mafuta na shilingi
milioni 122,000,000/= zisizokuwa na stakabadhi za EFD.
Aidha , Mkuu wa Mkoa aliagiza
kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni
pamoja kusimamishwa kazi kwa Watumishi au Watendaji wa Halmashauri hiyo
waliosababisha upotevu wa vitabu vya makusanyo ya mapato ya ndani na kutoa
taarifa katika ofisi yake ifikapo tarehe 30, Agosti, 2016. Katika Halmashauri
ya Wilaya ya Muleba hakuna Mtumishi aliyechukuliwa hatua.
MAAGIZO MENGINE.
Mkuu
wa Mkoa Mhe. Kijuu aliawaagiza Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Bukoba,
Muleba na Ngara kutojihusisha na kuchukua tenda au kufanya kazi za Halmashauri
zao ili kuondoa maslahi binafsi na Halmashauri zao. Pili, Wakurugenzi Watendaji
wote kuhakikisha wanafanya manunuzi yote kwa kwa wazabuni wenye stakabadhi za kielektroniki (EFD). Mwisho makusanyo yote ya mapato ya ndani ya
Halmashauri husika kukusanywa kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
Post a Comment