Wananchi mkoani KAGERA wametakiwa
kuacha kupotoshwa na watu kuhusu kutokea kwa tetemeko la ardhi ambalo limetokea
tarehe 10/9/2016 na kusababisha madhara mbalimbali.
Akizungumza na vyombo vya habari katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini PROFESSA JUSTIN NTALIKWA amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa tetemeko limesababishwa na imani za kishirikiana ambapo amebainisha kuwa tetemeko halihusiani na shughuli zozote za kibinadamu.
Amebainisha kuwa tukio la tetemeko la aridhi limeanzia kata ya Minziro ambapo amesema kuwa ni kilometa 10 kutoka ardhini amesema kuwa kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani KAGERA kunatokana na kuwa karibu na bonde la ufa.

Akizungumzia jinsi ya kujikinga na tetemeko linapotokea NTALIKWA amesema kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari na kuepuka kukimbia ambapo amesema tetemeko linatembea umbali wa kilometa 8 kwa sekunde moja huku akibainisha kuwa madhara makubwa yalitokana na watu wengi kukimbia ili kujiokoa.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala wa Jiorojia PRF ABUDULKARIMU MRUMA amesema kuwa tetemeko la ardhi linatokea kwa sababu za kijiorojia na hazisababishwi na kazi nyingine za kibinadamu.
.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wananzia vyombo vya moto pale tetemeko linapotokea ili kupunguza adhari.
Post a Comment