TAASISI za kifedha na mashirikia
mbalimbali wametakiwa kutokata tamaa katika kujitokeza kutoa msaada wa kusaidia
wahanga wa janga la Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani KAGERA na kusababisha
vifo 17 na zaidi ya watanzania 1000 wakiendelea kuishi kwa tabu kutokana nyumba
zao kubomoka.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoani Kagera ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Kaera Meja Jenerali Mstaafu SALIMU KIJUU ,wakati akipokea msaada kutoka katika taasisi ya Brac Tanzania ltd inayojishughulisha na shughuli ya utoaji mikopo hapa nchini.
Meja Jenerali KIJUU mbali na kutoa shukrani kwa taasisi hiyo,pia amewaomba wahisani hao kuendelea kuwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa limegubikwa na simanzi,kutokana na janga hio lililotokea na kusababisha vifo vya watanzania,pamoja na kufanya jamii ya wananchi wa mkoa wa Kagera kukosa mahali pa kuishi hadi sasa.
Kwa upande wake Mratibu wa kitengo cha masuala ya dharula wa taasisi ya Brack Tanzania Ltd CLARA LUCAS amesema msaada huo umetolewa na taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua changamoto kubwa inayolikabili taifa,kwani pamoja na shughuli za kibiashara zinazofanywa na taasisi yake ,pia usalama kwanza kwa wananchi ndilo jambo la msingi.
Amesema kuwa mchango uliotolewa umezingatia mahitaji ya msingi yanayohitajika kwa waathirika wa janga hilo,ambavyo watanzania wengi wamepoteza uhai pamoja na vitu vyao vingi ambavyo hali hiyo itawarudisha nyuma kiuchumi.
Amebainisha kuwa jumla ya shilingi milioni 20 za kitanzania zimetumka katika kuhakikisha mahitaji hayo yanapatikana,fedha ambazo zilihasidiwa kwenye kikao cha harambee kama sehemu ya mchango kutoka katika Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi hiyo mkoani KAGERA TIPU SULTANI ,amesema BRACK itaendelea kuwa bega kwa bega na uongozi wa mkoa chini ya kamati ya maafa lengo ni kuhakikisha wanashirikiana kutatua changamoto zitakazo jitokeza hasa kwa kipindi hiki ambacho mkoa unahitaji msaada wa hali ili kuwahifadhi waathirika wa jango hilo.
Hata hivyo SULTANI amefafanua kuwa mbali na msaada huo,Brack Tanzania ltd,bado inaendelea kukamilisha utaratibu wa kutoa msaada kwa wanachama wa taasisi hiyo walioathirika na tetemeko hilo,mpango unaotegemewa kutekelezwa hivi karibuni.
Post a Comment