Wazazi
na walezi wa
wanafunzi waliohitimu elimu
yao ya msingi
wametakiwa kuwafundisha elimu ya
kujitegemea kwa kipindi
ambacho watakuwa nyumbani
wakisubilia matokeo ya
mtihani wao walioufanya
mwezi huu amesema
kuwafundisha kujitegemea kutawasaidia
kwenye maisha yao ya
baadae.
Wito huo
umetolewa na Exvery Buguzi
diwani wa Kata
ya Nyakakika ambaye
alikuwa mgeni rasmi
katika maafali ya
15 ya shule
ya Kiingereza ya
Omukaliro ambayo ipo katika
kata ya Nyakabanga
wilayani Karagwe amesema
kuwa wanafunzi waliohitimu elimu
yao ya msingi
inabidi kuwafundisha kujitegemea
ili waweze kuwa wanajamii wazuri
wa baadae.
Amesema
kuwa hata wanafunzi
waliohitimu elimu ya
msingi mwaka huu
waendelee kujikumbusha waliofundishwa kama
maandalizi ya kuendelea
na masomo ya sekondari hapo
mwakani hivyo akawataka
wazazi na walezi
kujiandaa na hatua
hiyo ambayo ni
muhimu kwa watoto
wao kuendelea na ngazi
nyingine hatimaye wafikie
malengo na ndoto
zao.
Buguzi amesema
wanafunzi waliohitimu wajihadhari
na vitendo visivyokubalika katika
jamii kama uvutaji
bangi,ulevi,uzinzi na vitendo
vingine ambavyo haviendani
na mila na
utamaduni wa jamii
hivyo wanatakiwa kuepuka
visawishi hivyo.
Aidha amesema
kuwa ombi la wahitimu
waliolitoa kupitia risala
yao ya kutaka
shule hiyo iingizwe
kwenye mpango wa
umeme vijijini yaani
REA amehaidi kuendelea
kulifanyia kazi kwani
shule hiyo ni
taasisi muhimu inayowasaidia kuelimisha
watoto wa Tanzania
Akitoa neno
la shukrani Mtume
Mstaafu ambaye pia
ni mwenyekiti wa
Karadea Mathias Nzarombi
amesema wazazi na
walezi waendelee kuwa
na imani na
shule ya OMUKALIRO
kwani amazingira ya
kujifunzia na kufundishia
ni rafiki kwa
watoto na kuonya
wapinzani wao kutowapiga
vita visivyokuwa na
maana wala ugomvi
wowote.
Hata hivyo
waliohitimu mwaka huu
katika shule ya
Kiingereza ya Omukaliro
ni 31 ambapo wasichana
ni kumi na
wawili na wavulana
ni kumi na 19
Post a Comment