UBALOZI wa China,
Makampuni pamoja na Wananchi wa nchi hiyo wametoa msaada wa vitu
mbalimbali Vyenye thamani ya shilingi milioni 100 wa ajiri ya waathirika waliopatwa na tetemeko la ardhi
ili kuwasaidia katika makazi yao.
Akikabizi misaada
hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu SALUMU KIJUU
, Naibu Balozi wa nchi ya China ZHANG BIAO amesema Baloz wa
wa nchi hiyo DK Lu Youqing alizungumza na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania DK John Magufuli na kusikitishwa na tukio hilo.
BIAO amesema
kuwa,ubalozi kwa kuunganisha nguvu za pamoja na wananchi wa nchi hiyo na
kuitisha mkutano wenye kukusanya mfuko kwa waathirika wa tetemeko kwa
kununua vifaa ambavyo vitawasaidia kama , mahema,madawa chakula , maji na
blanketi.
Amebainisha kuwa,
kampuni ya ujenzi ya kichina iliyoko nchini china imetoa mifuko ya
saruji tani 80ikiwa China na Tanzania zimefanya ushirikiano katika shughuli
mbalimbali za kuijenga taifa katika karne iliyopita.
Kwa upande wake
mkuu wa mkoa wa KAGERA Meja Jenerali Mstaafu SALUM KIJUU , amesema
misaada hiyo aliyoipokea atahakikisha inawafikia walengwa wote bila
kujali itikadi za kikabila, siasa,
wala dini kwa taratibu aklizozipanga ili kufakisha zoezi hilo.
Aidha amesema tayari
misaada inaendelea kutolewa kutoka kwa wananchi mbalimbali wenye kuguswa na
tatizo hilo na tayari milioni 460 zimeingizwa katika akaunti ya kamati ya maafa
ya mkoa Benki iliyopo CRDB
inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba.
0152225617300. kwajili ya uchangiaji huo.
Post a Comment