Timu ya
Kamachumu Fc kutoka
wilayani Muleba imejipatia
mshindi wa magoli
3-1 dhidi ya Atukuzwe Fc
ambao ni wenyeji
wa wilaya ya
Karagwe katika mchezo
wa ligi ya
Taifa mkoa wa
Kagera ambayo inaendelea
kwa kituo cha
Karagwe moani Kagera.
Timu ya
Kamachumu Fc ilikuwa
ya kwanza kujipatia
goli dakika ya 3 kupitia
kwa mshambuliaji wa Joseph Mashoto baada ya
beki wa mwisho
wa Atukuzwe Ayoub Meshack
kuteleza na mshambuliaji
huyo kuwahi mpira
na kuachia shuti
kali lililomshinda mlinda
mlango Sadock Babwanga.
Atukuzwe Fc
waliongeza kasi ya
mashambulizi na kufanikiwa
kusawazisha goli hilo
dakika 18 baada
ya mabeki wa Timu
ya Kamachumu Fc
kushindwa kuondoa mpira
langoni mwao ambapo
ilikuwa piga ni
kupige ndipo mchezaji
wa Atukuzwe Fc Ibrahimu
Mbwilo Alipata nafasi
ya kumalizia mpira
huo.
Mchezaji huyo
Ibrahimu Mbwilo alisema
kilichowapelekea kupoteza mchezo
huo ni kutokana na
wachezaji wenzake kutojipanga
vizuri.
Kamachumu Fc
walijipatia bao la
pili dakika 38
kupitia kwa mshambuliaji Kayana
Kaiza baada ya kuwahi
mpira uliowashinda mabeki
wa Atukuzwe kuuondoa
katika eneo la
hatari hadi mapumziko
Kamachumu Fc goli
2 na Atukuzwe
goli 1
Kipindi cha
pili kilianza kwa
kasi kwa timu zote kufanya
mashambulizi ya mara
kwa mara ilikuwa
ni Kamachumu Fc iliyoweza
kujiongezea goli na
kujihakikishia ushindi
dakika 65 kupitia kwa
mchezaji Kayana Kaizaaliyepokea mpira
kutoka wingi ya
kulia na kumkuta
katika nafasi nzuri
ya kufunga.
Emanueli Byarufu
ambaye ni kocha
wa timu ya
Atukuzwe alisema maandalizi
yalikuwa ni hafifu
na kuongeza ilikuwa
ni kukurupuka hivyo
akasema anajipanga kwa
ajili ya mechi
ijayo.
Katika mchezo
ulioanza majira ya saa nane
mchana uliozikutanisha timu
ya Benaco stars ya
wilaya ya Ngara
na Chandimu stars
kutoka Manispaa ya
Bukoba ilishuhudi timu ya
Chandimu ikijipatia ushindi
wa goli 2-1 Benaco
ndio walikuwa wa
kwanza kujipatia goli
dakika ya 10 ya
kipindi cha kwanza
kupitia kwa Athuman
Nuru
Kuingia kwa
goli hilo kuliwaamusha
wachezaji wa timu
ya Chandimu wakaanzisha
mashambulizi ya mara
kwa mara langoni
mwa Benaco Stars
na kufanikiwa kusawazisha
goli hilo dakika 35
ya kipindi cha
kwanza na mfungaji
akiwa ni Evodius Kapilipili
Chandimu ilijipatia
goli la ushindi
dakika za lala salama
dakika 88 ya
mchezo kupitia kwa
mchezaji wao Fidel
Fidelisi akitumia makosa
ya mlinda mlango
aliyetoka langoni kuwahi
mpira bila ya
kuwasiliana na mabeki
wake.
Makochi wa
timu zote wamezungumzia
mchezo huo na
ligi kwa ujumla
wakisema waamuzi kuwa wametenda
haki na kuongeza
kuwa kiwanja bado
kwao ni tatizo
kwani hawajauzoea lakini
kwasababu wameishaingia vitani
hamna haja ya
kuogopa.
Emanueli Byarufu
ambaye ni kocha
wa timu ya
Atukuzwe alisema maandalizi
yalikuwa ni hafifu
na kuongeza ilikuwa
ni kukurupuka hivyo
akasema anajipanga kwa
ajili ya mechi
ijayo.
Post a Comment