Shilingi
milioni 300 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kashanda katika kata
ya Kabilizi wilayani Muleba ili kupunguza hadha inayowakabili wananchi wa
kijiji hicho.
Diwani wa
Kata ya Kabilizi Salmoni Karugaba
amesema kuwa fedha hizo zimeshapitishwa na baraza la madiwani katika bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa ajili ya
ujenzi huo .
Amesema
kuwa wakati wakisubiri fedha hizo kutoka
serikalini wananchi wameshaanza kujitolea mawe, mchanga na matofari kutokana na
hadha kubwa wanayoipata ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa kumi kufata
huduma ya afya.
Amesema
kuwa kata hiyo yenye vijiji vinne ina zahanati moja tu iliyoko katika kijiji
cha Kiwela hali iliyopelekea wananchi
wa vijiji vingine kutembea umbali mrefu kufata huduma ya afya .
Aidha
amesema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ukikamilika utaweza kuhudumia wananchi
wengi wa kata hiyo ambapo wanatarajia kuanza ujenzi huo mwishoni mwa mwezi January mwaka huu.
Post a Comment