Wazazi
na walezi wametakiwa
kuwapeleka watoto wao
amabao wamechaguliwa kuanza
masomo ya kidato
cha kwanza na
wale wanaotakiwa kuanza
elimu ya msingi
kwa mwaka huu
ili waweze kuanza
masomo mara moja.
Wito huo
umetolewa na diwani
wa Kata ya
Nyakabanga Justine Fidelis
wakati akizungumza na
Redio ya Jamii
Fadeco amesema wapo wanafunzi
wengi ambao hawajaripoti shuleni kwa
kuhofia kutokuwa na mahindi
ya uji hivyo
akawataka kuripoti mara
moja.
Amesema walimu
wanatakiwa kutowarudisha nyumbani
wanafunzi ambao wameisharipoti shuleni kwa
kile alichoeleza kuwa
ni michango ya mahindi
na mingineyo kwa
kufanya hivyo ni
kuwanyima haki yao.
Fidelis amewataka
walimu,wazazi,walezi pamoja na
viongozi kutimiza wajibu
wao katika kuwahudumia
wanafunzi hao ili
Taifa liweze kuwa
na kizazi kilichoelimika.
Hata hivyo wazazi wameaswa kuchangia mchango wa chakula
shuleni na kutosubilia viongozi kuchukua hatua za kisheria.
Post a Comment