Viongozi katika kata
ya Kabirizi wilayani Muleba
mkoani Kagera wametakiwa kutowavumilia wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto
wao shule.
Katibu
tawala wa wilaya ya Muleba
Benjamini Mwikasyege amesema hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Muleba wakati wa mkutano wa wananchi wa
kijiji hicho .
Mwikasyege
amesema kuwa serikali inaitaji
wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanakwenda shule hivyo
atakayeshindwa kumpeleka mtoto shule kwa makusudi serikali haitomvumilia na itapata nafasi ya kumsukuma kupeleka
mtoto shule
Amesema
kuwa viongozi wote kuanzia ngazi ya kijiji katika wilaya ya Muleba wameshapokea
maelekezo kutoka kwa mkuu wa wilaya kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda shule kwa muda muhafaka.
Wakati
akisoma taarifa ya kata hiyo kaimu afisa
mtendaji wa kata Nicodemus Mkata amesema kuwa
kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upungufu wa
walimu 44 pamoja na baadhi ya bara bara kupitika kwa shida.
Wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika kata hiyo ni 128 ikiwa
wavulana ni 64 na wasichana 64.
Post a Comment