Taasisi isiyokuwa
ya kiserikali ya Mhola imetoa mifuko
100 ya Saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule
ya msingi Kashanda iliyoko katika kata ya Kabirizi wilayani Muleba.
Mkurugenzi wa
Taasisi ya Mhola
Saulo Malauri inayotoa msaada wa
kisheria pamoja na kushugulika na maendeleo ya jamii hasa katika kitengo cha
malezi na makuzi ya watoto wameguswa
sana na upungufu wa madarasa katika shule hiyo.
Malauri amesema kuwa mtoto anaposomea katika
mazingira magumu inaweza kumpunguzia uwezo wa mtoto kupenda shule hivyo
wataendelea kushirikiana na viongozi wa kata hiyo kuhakikisha wanapunguza
changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wake
diwani wa kata hiyo Salmoni Karugaba amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa
vyumba 15 vya madarasa ambapo vyumba vinavyotakiwa kwa shule nzima ni 23 na
vilivyopo ni 8 tu.
Post a Comment