Jeshi la polisi
mkoani Geita limelazimika
kutumia nguvu kwa kupiga
mabomu ya machozi
ya kutoa machozi
kufyatua risasi za
moto hewani na
kupiga virungu wafuasi wa
chama cha demokrasia
na maendeleo chadema
waliokuwa katika stand
ya mabasi Geita
kwa ajili ya
kumpokea Waziri mkuu
mstaafu na mjumbe
wa kamati kuu ya
chama hicho EDWARD
LOWASSA aliyewasili mkoani humo kwa
ajili ya kampeini
za uchaguzi mdogo
katika kata ya
Nkome.
Tukio hilo limetokea
majira ya saa
kumi jioni wakati waziri
mkuu huyo wa
zamani Edward Lowassa akiwa kwenye gari lenye namba
za usajili T 771 DLA akikatiza
katika viwanja vya
stand ghafla kikosi
cha jeshi la
polisi kikiongozwa na
mkuu wa jeshi hilo
wilayani Geita Ally Kitumbo
kufika na kuwatawanya
wananchi.
Katika tukio hilo
pia waandishi wa
habari wawili Vallency Robert wa
Channel Ten na Joel Maduka
wa kituo
cha Redio STORM FM
wamepigwa na kuharibiwa
vifaa vyao vya kazi.
Hata hivyo
licha ya
Lowassa kupelekwa makao
makuu ya jeshi
la polisi mkoani
humo kwa ajili
ya kuhojiwa haikuelezwa mara
moja sababu ya jeshi
hilo kutumia nguvu kubwa.
Baadhi ya wananchi
waliozungumzia tukio hilo
wamelaani matumizi makubwa ya
nguvu ya jeshi la
polisi huku wengine wakilalamikia
waandishi wa habari
kuharibiwa vifaa vyao
na kupigwa.
Pia wananchi hao
wamelaani kitendo hicho
kwa kuwa Lowassa
hakuwa kwenye mkutano
eneo hilo bali
alikuwa akisalimiana na
wananchi wakati akielekea
kwenye kata ya NKOME kwa ajili
ya kampeini za uchaguzi mdogo.
Post a Comment