Shirika la
Jambo Bukoba linalohusika
na kuendeleza michezo
kwa shule za
msingi mkoani Kagera
leo limekabidhi mradi
wa visima viwili
vya maji vyenye
ujazo wa lita
70792 Vilivyogharimu zaidi ya shilingi
milioni 21 katika shule ya
msingi Kaaro ya
wilayani Kyerwa mkoani
Kagera.
Akitoa maelezo
ya chimbuko la
mradi huo mwalimu
mkuu wa shule
hiyo Deodatus Daudi
amesema ufadhili huo
ulitokana na shule
hiyo kushiriki michezo
ambayo inaandaliwa na
shirika hilo la
Jambo Bukoba ambapo
shule hiyo ilifanikiwa
kushinda kwa ngazi
ya wilaya na
kupata nafasi ya
kushiriki bonanza la
mkoa ndipo wakapata
mradi huo.
Meneja mradi
wa shirika la JAMBO
BUKOBA Beatrice Mbehoma
Bujune ambaye alimwakilisha
Imani Paulo ambaye
ni msimamizi wa
wilaya za Kyerwa
na Karagwe amewataka
wanafunzi pamoja na
jumuia ya shule
ya msingi Kaaro
kuvitunza visima hivyo
ili viweze kutimiza
lengo kuu la
kuwasaidia wanafunzi kuepukana
magonjwa yatokanayo na uchafu.
Amesema kuwa
JAMBO BUKOBA inahamasisha ushiriki
wa jamii ili
kuweza kuleta ufanisi
wa miradi hivyo
wakitunza visima hivyo
itasaidia kwa kiwango
kikubwa katika kuwaepusha wanafunzi
na uchafu usababishwao
na kukosa maji shuleni hapo na
lengo amesema ni
kuwasaidia kuwa na
mazingira bora ya
kujifunzia kwa kuwa
na afya bora.
Mgeni rasmi
Silvester Machera ambaye
ni Afisa Takwimu
na Vifaa wilaya
ya Kyerwa akimwakilisha Mkurugenzi
Mtendaji wa wilaya
ya Kyerwa amewataka
walimu,wanafunzi,Kamati ya shule
pamoja na wanafunzi
kutunza visima hivyo
vilivyojengwa kwa ufadhili
wa Shirika la
Jambo Bukoba ambao
wametoa asilimia 75
ya mradi huo
na jamii ikichangia
asilimia 25 za
mradi huo wa
visima viwili.
Naye diwani
wa Kata ya
Nkwenda Majaliwa John
ameiomba serikali kubadili
mfumo wa kutoa
zawadi ya barua
au ngao wanapofanya
vizuri kwenye taaluma na
badala yake waige
mfano wa jambo
BUKOBA wa kutoa
mradi ambao unahamasisha
shule nyingine kufanya
vizuri.
Aidha wanafunzi
nao walikuwa na
maoni juu ya kukamilika mradi
huo wa visima
kwasababu walikuwa na
shida kubwa ya
maji shuleni hapo
kabla ya kupata
mradi huo.
Mradi huo
wa visima viwili
vya maji vimegharimu
zaidi ya shilingi milioni 21
Shirika la Jambo
Bukoba limechangia sh milioni
15,971,250, Sawa na
asilimia 75 na jamii
ilichangia shilingi 5,325,750
sawa na
asilimia 25 za miradi hiyo
ya visima viwili.
Hata hivyo
wanafunzi na wazazi
wa shule hiyo
ya KAARO wameonesha furaha
yao kwa kukamilika
ujenzi huo wa
visima huku wakiomba
shirika la Jambo
Bukoba kuendelea kuwaunga
mkono kwani bado
wanazochangamoto nyingi.
Post a Comment