Rais
Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya
Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.
Awali
rais Magufuli ameivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
– TMAA na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa wakala huo, Mhandisi
Dominic Rwekaza kutokana na mianya ya upotevu wa mapato ya mchanga wa madini.
Maamuzi
hayo yamefanyika baada ya rais kupokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda
kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini -Makinikia
yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Rais
Magufuli anasubiri ripoti ya kamati ya pili iliyopewa jukumu la kuangalia
athari za uchumi na kisheria zilizotokea kipindi chote ambapo mchanga huo
ulikuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi.
Kamati
hizo mbili ziliundwa na Rais Magufuli baada ya mwishoni mwa mwezi Machi mwaka
huu kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya DSM na kubaini makontena ya mchanga
wa dhahabu yakisafirishwa nje ya nchi na kutilia shaka uhalali wa ukaguzi wake
na kuziagiza kufanya uchunguzi.
Post a Comment