Wananchi wametakiwa
kushiriki katika kutoa michango kwa ajili ya kukamiliza zoezi la upokeaji wa
mwenge katika wilaya ya KARAGWE ambao unatarajiwa kufika mwezi
wa nane mwaka huu.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha bajeti kilicho fanyika katika
ukumbi wa halmashauri ya wilaya KARAGWE ambapo wajumbe walio hudhulia kikao
hicho wameomba wananchi kuhamasiswa na kuhamasika katika zoezi la uchangiaji wa
michango.
Pia wajumbe wamesema
kuwa Taasisi na wafanya biashara mbalimbali watoe ushirikiano katika uchangiaji
wa michango kwa ajili ya kukamilisha shughuli za upokeaji mwenge.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ambaye ni katibu
Tawala wilaya ya KARAGWE INNOCENT NSENA amewaomba watendaji wa kata na vijiji
kuendelea kuihamasisha jamii ili kafanikisha
zoezi hilo.
Post a Comment