Wazazi na walezi mkoani
Kagera wametakiwa kuunga mkoano utoaji wa dawa za minyoo na kichocho kwa watoto
wao ii kuhakikisha kutimiza wajibu wao ili kufanikisha adhima ya serikali
kwa kukabiliana na magonjwa hayo.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu afisa Afya manispaa ya Bukoba GEREVASE ISHENGOMA wakati akizungumzia juu ya utoaji dawa unaoendelea shuleni kwa
watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 14.
Amesema kuwa magonjwa ya
Minyoo ya Tumbo mkoani Kagera bado yako juu ambapo utafiti uliofanyika mwaka
2016 katika baadhi ya shule za msingi Halmashauri nne shule iliyoongoza
ni kasosibakaya iliyoko halmashauri ya Bihalamulo kwa asilimia 84 ikifuatiwa na
shule ya msingi Ibuga iliyoko Ngara kwa asilimia 71.
Hata hivyo ISHENGOMA
amesisitiza kuwa kabla ya watoto kupewa dawa watoto wanapaswa wawe wamekula
kabla ya masaa mawili pamoja na kushiba vizuri ili kuepusha changamoto
zinazoweza kujitokeza.
Post a Comment