Jumla
ya wanafunzi 1057 wa shule ya msingi Kayanga Wilayani Karagwe wamepata dawa ya
kinga na tiba ya kichocho na minyoo.
Akizungumza
na chombo hiki mwalimu Mkuu wa shule hiyo Oswardi Maliseli amesema Zoezi
la utoaji wa dawa ya kinga na Tiba ya ya kichocho na minyoo katika shule yake limeanza mapema leo
asubuhi na kuamalizika vizuri kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Amesema
kabla ya kuanza kupata dawa hiyo,wanafunzi waliokuwa na umri wa kupata dawa
hiyo ,wameanza kula chakula kama maelekezo yalivyotolewa kutoka sekta ya Afya
,ambapo chakula wamekipata shuleni ,kilichochangwa na wazazi wa watoto husika.
Kwa
Upande wa wanafunzi baada ya kupata dawa hizo wameeleza kumeza dawa hizo chini
ya ulinzi wa walimu wao ili wasisitupe na hakuna madhara yaliyojitokeza kwao.
Wamesema
,baada ya kumeza dawa hizo walimu waliwaonyesha sehemu ya kupumzika na kuwataka
wasicheze mapaka dawa itulie ndani ili kuepuka baadhi ya watu wenye
kichefuchefu kutapika.
Aidha
baadhi ya wazazi walioongea na kituo hiki ,wamesema serikali imefanya vizuri
kuwapatia dawa watoto wao,kwani ni njia
bora ya kulinda afya zao na kusema kuwa swala hili linawapa imani ya kuwa na kizazi kisichoshambuliwa na magonjwa
kulinda ili kuendeleza jamii iliyosafi na salama.
Post a Comment