Kaya 200 zilizolima
katika vyanzo vya maji katika kijiji cha Mikale na Kiwela katika kata ya
Kabilizi wilayani Muleba mkoani Kagera zimepewa wiki mbili kuondoa mazao yao
katika vyanzo hivyo.
Afisa kilimo wa
vijiji hivyo viwili Benedicto Karoli
amesema kuwa wameshafanya utafiti katika vijiji hivyo na kubaini kuwa kuna kaya
mia 2 ambazo zimelima katika vyanzo vya maji.
Karoli amesema kuwa wananchi hao wanatakiwa
kuacha tabia ya kulima katika vyanzo vya maji kwani kwa kufanya hivyo ni
kinyume na sheria ambapo wananchi wanatakiwa kukaa mita 60 kutoka katika vyanzo
vya maji ili kusaidia kutunza mazingira.
Amesema kuwa kila
mwananchi anatakiwa kutunza mazingira yanayomzunguka kwani kwa kufanya hivyo
itasaidia kutunza vyanzo vya maji katika vijiji hivyo.
Aidha amesema kuwa
kwa watakaoshindwa kutoa mazao yao katika vyanzo vya maji ndani ya wiki mbili
hizo zilizotolewa watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Post a Comment